Friday, May 26, 2017

Mzee aliyebuni na kuchora Nembo ya Taifa apatiwa matibabu na Serikali


Serikali ya imelazimika kumuhamishia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Mzee Francis Maige Ngosha aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Amana kwa kipindi cha siku moja kwaajili yakupatiwa matibabu zaidi.

Akitoa tamko la serikali Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Khamisi Kigwangalla amesema mzee huyo ambaye ni mmoja wa wachora Nembo ya Taifa amesema wameamua kumuhamishia katika hospital hiyo ya Taifa Muhimbili ili kufanyiwa uchunguzi wa kina na wataalamu wa magonjwa mbalimbali ili kubaini na kutibiwa.

Dkt. Kigwangalla amesema serikali itahakikisha inampa tiba kamili na malezi kwa kuzingatia haki ya kuishi ya binadamu na kuthamini mchango wa wazee na waasisi wa taifa.

Kwa upande wake daktari bingwa wa magonjwa ya dharura kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt. Juma Mfinanga amesema wanasubiri majibu ya vipimo wanavyomchunguza na pindi watakapobaini tatizo atapatiwa matibabu yake.

Kwa upande wake Francis Maige Ngosha ambaye ni mmoja wa wachora Nembo ya Taifa ameishukuru serikali na jami iliyokuwa ikimlea kwa miaka yote bila malipo.
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )