Friday, May 12, 2017

PICHA: Maporomoko ya mawe yafunga barabara Tanga

Jeshi la Polisi mkoani Tanga jana  lilifunga barabara ya kutokea Dar es salaam kuelekea Arusha kufuatia eneo la Mombo mkoani Tanga kuangukiwa na maporomoko ya mawe pamoja na matope na kusababisha athari kwa baadhi ya magari

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi mkoani humo Benedict Wakuyamba  alisema, maporomoko hayo yalisababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Mkoani humo na maeneo mbalimbali nchini

"Hali ya mvua imeendelea kunyesha na kufukia barabara eneo la Mombo kutokea Dar es salaam kuelekea Arusha ambapo matope na miti vimesombwa na kukwama barabarani hali iliyokwamisha magari makubwa kwa madogo kusafiri kupitia eneo hilo..

"Niwaombe abiria au wananchi kwa ujumla kama hawana ulazima wa kusafiri kwenda mikoa ya Kaskazini ni vizuri wakatulia kwa siku mbili tuone hali inakwendaje kwa ajili ya usalama wao". Alisema Kamishna Msaidizi Benedict

Kwa upande mwingine Kamishna huyo alisema TANROADS na Jeshi la Polisi mkoani humo wanaendelea kusaidia kuondoa magogo na tope zilizosakama katika barabara ili kunusuru hali ya usafiri.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )