Monday, May 8, 2017

Rais Magufuli: Napata Machungu na Majonzi Ninapoyaona Haya Majeneza ya Watoto Wetu

Rais Dkt Magufuli ameshindwa kujizuia na kusema kuwa amekumbwa na majonzi makubwa baada ya kuona majeneza 35 ya wanafunzi wa Shule ya Lucky Vicent ya jijini Arusha waliofariki katika ajali ya basi wilayani Karatu Mkoani Arusha.

Rais Magufuli ameyasema hayo wakati miili ya wanafunzi 35, walimu 2 na dereva mmoja ikiagwa katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha na kisha kusafirishwa maeneo mbalimbali kwa ajili ya maziko.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Rais Dkt Magufuli aliandika, “Nimepatwa na uchungu na majonzi makubwa ninapoyaona majeneza ya watoto na walezi wao waliopoteza maisha katika ajali ya basi huko Arusha .”

“Tumewapoteza mashujaa wetu ktk elimu. Tuwaombee na tuendelee kuwa na subira, uvumilivu na ustahimilivu 2/2.”

Aidha, Rais Dkt Magufuli amewasihi wa Tanzania kuendelea kuwa wamoja wakati wakiomboleza tukio hili kubwa lililoikumba nchi na kuacha simanzi miongoni mwa watu wengi.

“Tunapoomboleza vifo vya wapendwa wetu tuendelee kuwa wamoja. Mungu ibariki Tanzania.”
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )