Friday, May 5, 2017

SORRY MADAM -Sehemu ya 59 & 60 (Destination of my enemies)

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWAILIPOISHIA

ILIPOISHIA
. Taratibu akapiga hatua za uwoga, akaingia, ndani, mtoto huyo akaufunga mlango huo ulio kaa kama ukuta.
“Umepajuaje huku?”
“Babu yangu ndio alinionyesha huku”
“Babu yako”
“Ndio.”
“Kwanza unaitwa nani?”
“Naitwa Soroo”
Walizidi kushuka chini, wakakuta kordo moja ndefu iliyo jaa taa pembeni kwa juu,  mbele yake kwa mbali kuna mlango wa kuingilia kwenye chumba kimoja tu kilichopo kwenye eneo hilo. Wakazidi kupiga hatua, wakiwa umbali fulani kutoka kilipo chumba hicho, taa zikaanza kufifia. Wote wakajikuta wakiogopa, gafla taa zote zikazima na kujikuta wakipiga kelele za woga kwani giza zito lilitanda kwenye mboni za macho yao.

ENDELEA
   Haikupita hata dakika moja taa hizo zikawaka, wote wakanyamaza na kushusha pumzi zao. Kila mmoja woga ulimtawala.
“Turudi zetu”

Phidaya alizungumza huku akimshika mkono Soroo, habari ya kwenda alipo Black Shadow, ikayayuka moyoni mwake, hakutamani kuona anafia kwenye sehemu hiyo chini kabisa ya ardhi. Wakaanza kutembea kwenye kordo kurudi walipo tokea tena safari hii waliongeza hata mwendo wa kutembea. Kila mara Phidaya alitazama nyuma kuona kama kuna kitu kinakuja. Wakazipandisha ngazi kwa haraka, Soroo akafungua mlango, wakapita na kutokezea katika choo walicho ingia.
Wakarudishia kila kitu sehemu yake, na kutoka kwenye mabweni hayo. Moja kwa moja wakarudi katika sehemu ya mkusanyiko walipo watoto wengine pamoja na walezi wao.
“Mumefanikiwa kuona kitanda chake?”
Mlezi mmoja alimuuliza, huku akiachia tabasamu pana usoni mwake.

“Ndio, nimefurahi sana kuona mabweni yao. Nitahalkikisha kwamba tunaongeza mabweni ili mumweze kuchukua vijana wengi wamaoishi kwenye maisha magumu”
“Tutashukuru sana madam”
“Nipo pamoja nanyi. Naona muda wangu hautoshi basi ngoja niwaache muendelee na majukumu”
Phidaya alijikaza kuzungumza hivyo, ila mwili mzima alihisi kama umekufa ganzi kwa woga. Phidaya akamuaga Saroo, na kumuahidi atarejea kisha akangia kwenye gari lake na kuelekea hotelini wanap ishi Shamsa na mwenzake. Wakawakuta wakiwa wanafanya mazoezi ya viungo. Wakasalimiana kwa furaha, huku Phidaya akimbusu Shamsa kwenye paji la uso.

“Vipi mbona mupo kwenye mazoezi makali?”
“Kuna kitu mama nahitaji uweze kunisaidia”
“Kitu gani hicho?”
“Nihitaji kutafuta ukweli kuhusiana na kitu ambacho kilikupata wewe kwa maana inavyo onekana hukumbuki mambo ya nyuma”
Shamsa alizungumza huku akimtazama Phidaya usoni, anaye onekana kumsikiliza kwa umakini sana.
“Nahitaji kufahamu maeneo ambayo dokta Ranjiti anapenda kuyatembelea?”
“Kwa sasa yupo Korea Kusini”
“Mama hujanielewa swali langu, yaani sihitaji kujua yupo wapi ila nahitaji kufahamu maeneo anayo penda kwenda kutulia”

“Kusema kweli sifahamu, huwa Ranjiti muda mwingi anapenda kuutumia akiwa hospitalini, na hata akitoka ni sehemu chache sana ambazo anakwenda na kurejea”
“Au labda Yan yule rafiki yake aliye kuwa naye katika chumba cha Black Shadow anaweza kufahamu maeneo ambayo Ranjiti anapenda kuyatembelea kwa sana”
“Eheee umenikumbusha mama hivi siku ambayo uliwasikia wakizungumza kwenye chumba cha Black Shadow, Yan si alihusika?”
“Ndio lihusika”
“Basi mama nimeshapata kwa kuanzia, kila jambo kwa sasa litakwenda sawa, niachie mimi hiyo kazi”

“Sawa. Ila unataka kufanya nini?”
“Mama kila kitu nimekuambia niachie mimi, nikiimaliza kazi yangu nitakuletea ripoti kamili”
“Sawa ila kuwa makini kwa maana hawa watu mimi wala siwaamini sana”
“Usijali mama yangu, hivi nyumbani kwa Yan si unapafahamu?”
“Ndio napafahamu”
Phidaya akamuelekeza Shamsa na Sa Yoo nyumbani kwa daktari Yan, kutokana Sa Yoo ni mwenyeji sana katika nchi hiyo ya Japan, eneo hilo alilifahamu.
                                                                                                     ***
   Majadiliano ya dokta Ranjiti, dokta Yan na Kim ndani ya ndege, yalimchanganya rubani wake ambaye alikuwa ndani ya ndege hiyo pasipo bosi wake kuweza kufahamu. Mpango wa kwenda kumteka Black Shadow, kwenye hospitalini na kwenda kumuua kwa kumchoma moto. Aliweza kuisikia vizuri, rohoni mwake akajikuta akishindwa kuvumilia kuona tukio hilo likiwa linatendeka.

Mzee Yo, aliyasikiliza mazungumzo hayo hadi mwisho, bosi wake alipo ondoka katika eneo la karakana kwa haraka akashuka kutoka ndani ya ndege. Hakumuaga mtu, akapanda pikipiki yake, iliyo mpeleka moja kwa moja hadi nyumbani kwake. Kichwani kwake mawazo mengi yalizidi kukiandama kichwa chake, kila alipo jaribu kufikiria jinsi ya kumuokoa Black Shadow, alijikuta akishindwa kupata jibu kabisa.

“Nitafanyaje wakati kazi hii ni hatari sana. Laiti bosi akitambua nitakuwa sina kazi na pia anaweza kuniua”
Mzee Yo alizungumza peke yake akiwa chumbani kwake amejiinamia kwenye sofa lake. Japo ni rubani wa muda mrefu katika kampuni ya dokta Ranjiti, ila leo ndio aliweza kufahamu kwamba dokta huyo ni mtu katili sana. Kila alipo mfikiria Black Shadow, kijana ambaye ana ujuzi mkubwa wa kupigana, hadi akamteka kihisia, hakukubali kuona anakufa mikononi mwa dokta Ranjiti ambaye amepewa jukumu la kumtibu. Hakuhitaji kufahamu ni kitu gani ambacho Black Shadow amekifanya kwa daktari huyo ila kitu alicho kihitaji ni kuhakikisha kwamba kijana huyo anakuwa hai.

Kwa haraka haraka, akilini mwake akafikiria ni mtu gani anayeweza kumsaidia katika kazi hiyo, kura yake ikatua bibi Eyna. Mwanamke aliye kuwa na mahusiano naye miaka mingi ya nyuma, kabla hawajatengana. Akakumbuka kwamba bibi Eyna anafanya kazi katika hospitali ya dokta Ranjit, kwa haraka akachukua kitabu chake cha kuhifadhia kumbukumbu. Akaanza kufungua kurasa kadhaa, akiitafuta namba ya simu ya bibi huyo. Akabahatika kuipata namba hiyo. Akaingiza namba hizo kwenye simu yake ya mkononi, akaiweka sikioni simu yake na kusikiliza, kwa bahati nzuri simu hiyo iliita kwa muda kisha ikapokelewa.

“Habari yako Eyna”
Sauti ya Mzee Yo, haikuwa ngeni masikioni mwake, moyo wa bibi Eyna ukajikuta ukikubwa na furaha kubwa.
“Safi tu Yo habari za siku nyingi?”
“Safi upo wapi kwa sasa?”
“Nipo kazini”
“Naweza kuja kukuona mpenzi?”
“Mmmm jamani, mpenzi si usubiri nikitoka”
“Hapana ni muhimu sana, nahitaji kukuona mida hii nina hamu sana na wewe”
“Waooo njoo basi nakusubiria”

Mzee Yo, akakata simu baada ya kutumia mameno ya ulaghai kwa mpenzi wake huyo, ambaye aliweza kuachana naye kutoka bibi Eyna enzi za ujana wake hakutulia na mwanaume mmoja. Ndani ya dakika thelathini akawa amefika katika hospitali ya dokta Ranjiti, hakupata tabu sana kuweza kukutana na Bibi Eyna, ambaye alimkumbatia kwa furaha mara baada ya kumuona.
Japo ni mzee ila bibi Eyna bado ana hulka za ujana, hakusita kumpiga mzee Yo busu la mdomoni.
“Baby nimefurahi kukuona jamani”
“Hata mimi, ila unaonekana una joto kali”
Mzee Yo, alitania, huku kiganja chake akiwa amekiweka shingoni mwa bibi Eyna.

“Ni joto la kulimisi penzi lako?”
“Kweli?”
“Ndio”
“Ninaweza kukupatia ubaraidi wakati huu?”
“Mmmm jamani, mbona unanisisimua”
“ Sikusisimui ila ninacho kizungumza nina kimaanisha baby”
Mzee Yo, aliweza kuutambua udhaifu wa mwanamke huyo, kwani anapenda sana ngono kuliko hata kula ndio maana walishindwana kipindi cha ujana wao.

“Sasa hapa tutafanyia wapi mume wangu?”
“Kwani hakuna chumba cha siri tukafanya mambo?”
Bibi Eyna akaichekecha akili yake kwa haraka huku akifikiria sehemu gani, akakumbuka kwamba ndani ya hospitali hapo kuna vyumba vya siri ambavyo vipo ardhini ila havitumiki kwa muda mrefu sasa. Hakujua uwepo wa Black Shadow ndani ya moja ya vyumba hivyo, kwani uwepo wa Black Shawod ni siri iliyopo kwa madaktari wakubwa tu, hata madaktari wengine hawatambui.

“Hembu kaa hapo niandae mazingira kisha naja kukuchukua”
“Mazingira gani baby”
“Ngoja kuna vyumba vipo huko ardhini nahisi huko kutatufaa mpenzi wangu”
Bibi Eyna akaondoka katika eneo hilo akiwa mwingi wa furaha na amani sana, haraka haraka akaelekea kweye ofisi ya dokta Ranjiti akagonga kwa muda, hakuitikiwa, akausukuma mlango na kukuta haujafungwa kwa funguo.

Akachungulia ndani hapakuwa na mtu, akaelekea ofisi ya Phidaya, akagonga pia akukuta hakuna mtu. Akaelekea katika ofisi ya dokta Yan, ambaye ni msaidizi wa dokta Ranjiti naku huko pia hakukuta mtu. Siku hiyo akajiona ni mtu mwenye bahati sana, akarudi sehemu alipo muacha Mzee Yo. Akamuomba amfwate kwa nyuma.

Wakaingia kwenye chumba ambacho kina lifti iliyo washusha chini. Kitendo cha kufika eneo hilo, bibi Eyna akamkumbatia kimahaba mzee huyo na kuanza kumpiga mabusu mfululizo.
“Baby tulia kwanza tuchunguze kuna weza kukawa na mtu humu akatuona ikawa tatizo”
“Baby hakuna mtu bwana”

Mzee Yo, akitazama saa yake ya mkononi inamuonyesha ni saa mbili usiku. Muda wa Black Shadow kuja kutolewa kwenye eneo hilo ni saa nne usiku. Kutokana na yeye ni mwanaume rijari, hakuona vibaya akampatia haki bibi Eyna, haraka haraka ili kuzidi kumchanganya na kumuweka karibu pale ataka anza kufanya mpango wake, kwa maana anatambu lazima Black Shadow yupo kwenye chumba hicho, kutokana alisikia jinsi Kim alivyo kuwa akielekezwa chumba alicho Black Shadow, kila alama aliyo isikia kwenye ndege ipo kwenye moja ya mlango.

Kwa haraka, akalipandisha gauni la bibi Eyna hadi kifuani, akamshusha chupi aliyo ivaa, na yeye akashusha suruali na nguo yake ya ndani. Agamshikisha ukuta bibi Eyna, bila hata maandalizi, ya kumuandaa mwenza wake, akaanza kumpa haki yake.

Bibi Eyna, akaanza kutoa miguno ya mahaba, kwa kasi ambayo anakwenda nayo Mzee Yo, ilimfanya apagawe na zaidi ya mara nne, bibi Eyna alijikuta anafika kileleni. Mzee Yo akafunga goli lake dakika kumi baada ya mchezo kuanza.  Bibi Eyna akajikuta akikaa chini kwa jinsi alivyo choka kwani ni muda mrefu hajakutana na mwanaume wa kumpeleka kasi namna hiyo.

Mzee Yo akapandisha nguo zake, akajiweka sawa, bila ya kupotaza muda akaanza kufungua mlango ambao alisikia maelekezo yake yakiwa yanatolewa. Kweli akamkuta Black Shadow akiwa amelala kwenye kitanda hicho akiwa hajitambui, ili kuhakikisha ni yeye akamsogelea karibu, kinyago cha Black Shadow alicho kivaa kilimuhakikishia kwamba ndio mwenyewe.
“Haaaa…….!!!”
Sauti ya Bibi Eyna ilimstua akageuka na kumkuta akiwa amesimama kwenye mlango huku mdomo wake ukiwa mdomoni.
“Shiiiii”
“Huyo si ndio mgonjwa mbaye alivamiwa majuzi?”
Bibi Eyna alizungumza huku akienda kumtazama Black Shadow kitandani alipo lala.
“Nahitaji kumtorosha hapa hospitalini”

“Kwa nini?”
“Kuna watu wanahitaji kumuua”
Macho yakamtoka bibi Eyna kwa kushangaa
“Usishangae, dokta Ranjiti  anahitaji kumua, sasa nahiyaji tumtoe kiakili pasipo mtu mwengine kutambu”
“Si unanitafutia matatizo jambo hili likijulikana”
“Una nipenda ua hunipendi?”
“Nakupenda”
“Fanya kama ninavyo hiaji akiendelea kukaa hapa ninaimani wakuu wako watakuja kumuua”
“Ina maana dokta Ranjiti anahitaji huyu kijana kumuua?”
“Hilo ni jibu na si swali, hatuna muda wa kupoteza nilaziama kumtoa humu ndani”

“Sasa utambeba wapi,  kwa maana hivi hivi ataonekena”
Mzee Yoo akatoka kwenye chumba hicho, akaingia kwenye chumba kingine, ambapo akakuta maboksi mengi makubwa yakiwa yamepangwa, akalifunua boksi moja na kukuta likiwa halina kitu ndani yake, kwa ukubwa wa boksi hilo akamini kwamba litamsaidia katika mpango wake.
Akarudi nalo kwenye chumba alipo Black Shadow, akamkuta bibi Eyna akiwa amelifunua shuka lililo kuwa limemfunika Black Shadow nusu mwili, msho uliopo kwenye mbavu zake ukmfanya Mzee Yoo aumize kichwa kufikiria jinsi ya kumuingiza humo.
“Unataka kumingiza kwenye boksi?”
“Ndio”

 
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )