Sunday, May 14, 2017

SORRY MADAM -Sehemu ya 61 & 62 (Destination of my enemies)

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWAILIPOISHIA

ILIPOISHIA
Gafla hata kabla hajaanza kuvuka barabara, gari moja jeusi aina ya haisi, likasimama sehemu alipo simama Phidaya, wakashuka watu wawili walio valio vinyago vyeusi wakamata kwa nguvu na kumuingiza ndnai ya gari hilo na kuondoka naye kwa nguvu, kitendo kilicho shuhudiwa na Eddy pamoja na Shamsa, kupitia kwenye kioo kikubwa akiwa ndani ya duka hilo. Eddy akavuka kwa kasi bilia kujali magari yanayo pita kwenye barabara hiyo huku Shamsa naye akitoka kwa kasi nje, wote wawili wakajikuta wakisimama katika sehemu aliyo tekewa Phidaya na macho yao wakilishuhudia gari hiyo ikitokomea kwa mbali.

ENDELEA
  Kila mmoja alishusha pumzi, akifikiria cha kufanya,  Sa Yoo, akatoka huku akiwa ameshika mfuko ulio jaa nguo
“Kumetokea nini?”
Wote wawili wakamtazama Sa Yoo, ambaye kidogo akaonyesha mstuko baada ya kumtazama Eddy usoni, Eddy naye aliweza kumtambua Sa Yoo.

Ni binti aliye weza kumsaidia na aliachana naye siku walipo kwenda hospitalini. Jinsi Sa Yoo alivyo kuwa akimtazama Eddy machoni huku akimsogelea taratibu, kukamfanya Shamsa naye kumtazama mwanaume aliye kuja kusimama naye hapo akionekana aliliona tukio hilo. Macho yalimtoka Shamsa, mapigo ya moyo kidogo yakaanza kumenda mbio, akatamani kuliita jina la Eddy ila kigugumizi cha gafla kikamfanya aishie kupanua mdomo wake akimshangaa Eddy.
“Wewe si Eddy?”

Sa Yoo alizungumza huku akibonyea kidogo na kuchungulia Eddy, usoni mwake kwani kofia yake iliuziba uso wake kwa kiasi kikubwa. Japo amevaa ndevu za bandia ila Sa Yoo aliweza kumtambua haraka na kulitaja jina lake. Eddy hakujibu chochote iku kuwazugisha akajifanya akigeukia kule lilipo kuwa linaelekea gari.

Macho ya Eddy yakawashuhudia askari wawili wakija katika eneo hilo, Eddy hakuona haja ya kuendelea kusiamam hapo kwani alitambua askari hao wanaweza kumuharibia siku yake, akatazama barabara pande zote mbili hapakuwa na gari inayo kuja akavuka kwa haraka, Shamsa akataka kumfwata ila Sa Yoo akamzuia kwani kuna gari ambayo ilikuwa inapita kwa kasi na endapo angepita basi angegongwa.

“Heii miss, mbona huangalii magari?”
Askari mmoja alizungumza huku akimtazama Shamsa usoni mwake.
“Ohoo samahani maafisa, kidogo ana mawazo?”
“Kwani kuna tatizo kati yenu?”
Askari mwengine aliuliza huku akimtazama Eddy aliyekuwa akipanda pikipiki, akiondoka na mzee Yo.
“Ahaaahah hakuna”
Sa Yoo yeye ndio alikuwa mjibuji wa maswali hayo, kwani Shamsa wakati wote macho yake aliyaelekezea kwenye pikipiki iliyo kuwa ikitokomea upande wa pili, ikakunja kona kulia na hakuiona tena.

“Madam una mawazo sana”
“Eheeee”
Shamsa akastuka kutoka kwenye dibwi zito la mawazo akimfikiria mtu aliye muna ni Eddy, swali alilo jiuliza mbona mtu huyo hakuweza kusema kitu chochote zaidi ya kuondoka. Wazo la Phidaya kutekwa likamjia upya akilini mwake.

“Mama ametekwa”
“Ametekwa, ametekwa saa ngapi si alitoka nje kuzungumza na simu?”
“Sa Yoo kuwa muelewa mama ametekwa”
Habari hiyo ikawastua hadi polisi hao, wakaanza kumuhoji maswali Shamsa, akaelezea jinsi alivyo weza kushuhudia, askari mmoja akaondoka kulifwata gari lao na kurudi nalo katika sehemu alipo mwezake kwa ajili ya kumchukua Shamsa kwenda naye kituoni kutoa maelezo yakutosha.

Shamsa akamkabidhi Sa Yoo funguo ya gari la Phidaya na kumuomba awafwate kwa nyuma, na awasiliane na Lee Si na kumpa habari ya kutekwa kwa Phidaya. Sa Yoo akaingia kwenye gari la     Phidaya akiwa na fuko lake lililo jaa nguo nyingi. Akaanza kulifwata gari la polisi kwa nyuma, akatoa simu kwenye mfuko wa jinzi alilo livaa, akatafuta namba ya Lee Si kwenye orodha ya majina yake kweney simu hiyo na kumpigia, siku kwa mara ya kwanza ikaita na kukatwa, akapiga tena akakuta simu ikiwa imezimwa kabisa.
“Mmmmmmm……….”
Aliguna Sa Yoo na kuirudisha simu yake mfukoni na kuzidi kulifwata gari la polisi kwa nyuma hadi katika kituo kikuu cha polisi nchini Japani
                                                                                           ***
   Mawazo mengi yakazidi kukisonga kichwa cha Eddy, akajiona ni mkosaji kushindwa kuzungumza chochote mbele ya Shamsa, ili kujulikana. Kila alipo likumbuka busu la Shamsa, machozi yakamtoka akatambua ni wazi kwamba mwanaye huyo amempenda, pasipo kujua kwamba amempenda mtu anaye muheshimu kama baba yake japo hakumzaa. Jambo jingine lililo zidi kumchanganya Eddy akilini mwake ni uwepo wa Phidaya nje ya duka ambalo Shamsa aliweza kutoka.
‘Ina maana Shamsa na huyu nesi wanajuana?’
‘Na wamejuana vipi? Au ni Phidaya mke wangu?’
‘Mmmm Phidaya wangu amekufa huyu si yeye’

Eddy aliwaza huku akiwa juu ya pikipiki ya Mzee Yo, ambaye ndio dereva, wakafika kwenye moja ya soko huku Eddy mara zote akiwa sura yake ameiweka chini, hakuhitaji kuinyanyua isije watu wakaistukia kama Sa Yoo ameweza kumtambua kwa haraka kiasi kile japo kuwa ameweka ndevu za bandia usoni mwake basi akaamini kwamba hata mtu wa kawaida anaweza kumtambua na ikawa ni tatizo kubwa kwake kutokana donge nono la zawadi ambalo wamelitangaza polisi, kila mwananchi aliamini kwamba analitamani kulipata.

Baada ya kununua manunuzi walio ona yanatosha, wakaanza safari ya kwenda mapangoni wanapo ishi. Mzee Yoo, alikituma kipindi hichi cha likizo vizuri kukaa mapangoni akifurahia uwepo wa Eddy aliye mchukulia kama mwanaye wa kumzaa
                                                                                             ***
    Kitendo cha Phidaya kumueleza Lee Si mpango wa Shamsa wa kutaka kumvamia dokta Yan usiku, hakujua ni jambo gani ambalo lingeweza kutokea. Lee Si alipo maliza majukumu ya kumrudisha bosi wake nyumbani kwake, akarudi hotelina ambapo amepangishiwa kwa muda na boasi wake hapo, kujificha kuepuka uvamizi wa Kim, ambaye hadi sasa hivi atambui yupo wapi wala ana mpango gani ambao anahitaji kuweza kuufanya.

Lee Si, akachukua bastola yake, iliyo jaa risasi za kutosha, akaifunga kiwambo cha kuzia sauti alipo, hakikisha kwamba majukumu yake yamekamilika, akajilaza kitandani kwake, mara kwa mara macho yake akawa anayatupia kwenye saa ya ukutani. Ilipo jiri saa nne kamili usiku akanyanyuka kitandani, akavaa mavazi meuzi, kisha akachukua koti lake kubwa jeusi na refu, akilivaa linamfika magotini.
Alipo hakikisha yupo vizuri akashuka hadi gorofa ya chini, akaelekea kwenye maegesho ya magari, akaingia kwenye gari lake na safari ya kueleka kwa dokta Yan ikaanza.

Akalisimamisha gari lake mbali kidogo na ilipo nyumba ya dokta Yan, akalivaa koti lake pamoja na miwani nyeusi. Akaanza kutembea kwa tahadhari hadi karibu kabisa na yumba ya dokta Yan. Kitu kilicho mtisha ni kukuta walinzi wakiwa wamelundikwa kwenye stoo, hawajitambui, machale yakaanza kumcheza na kutambua kwamba Shamsa si msichana wa kawaida kama alivyo kuwa akimchukulia hapo awali, kwani ni yeye pekee ndio alikuwa na mpango wa kufika katika nyumba hiyo.

Akajibanza kwenye moja ya ua alipo muona dokta Yan akishuka kwenye gari lake, akataka kumvamia ila akasita alipo muona dokta huyo akiwa amejawa na wasiwasi mwingi sana.  Alipo muona dokta huyo akiingia ndani ya gari lake na kutoka na bastola akatambua kwamba lazima daktari Yan atakuwa ameshtukia hali inayo endelea. Kitu kingine alicho hitaji kujua ni nani aliye ifanya kazi hiyo ya kuwapiga walinzi, japo ana muhisi Shamsa, basi akahitaji kudhibitisha kwamba ni yeye, au laa.

Akanyata hadi kwenye dirisha, la kioo, akasikiliza jinsi dokta Yan akijitetea, akaisikia pia sauti ya Shamsa, ila katika sehemu alipo simama hakuweza kumuona Shamza zaidi ya dokta Yan, aliye anza kupiga magoti taratibu.

Lee Si, hakuhitaji siri ambayo ipo kati ya bosi wake na mke wake iweze kutoka, kwani anaitambua vizuri sana, akaikoki bastola yake vizuri, akavuta jicho moja, akakiweka kichwa cha dokta Yan katikati ya shabaha yake, na kufyatua risasi moja iliyo tua kichwani mwa dokta Yan na kumuangusha chini na kufa hapo hapo.

Hapakuwa na mlio wa risasi hiyo iliyo kuwa ikitoka kwenye bostola yeke kwani tayari alisha ifunga kiwambo cha kuzuia risasi. Kwa haraka akaondoka na kukimbilia kwenye gari lake, akaondoka kwa kasi na kurudi zake hotelini, kuhakikisha kwamba Shamsa hawai kufika kabla yake.
Akafika hotelini, kwa haraka akapandisha gorofani kwake huku koti lake akiwa amelishika mkononi, akaingia chumbani mwake, akatoa simu yake mfukoni na kumpigia dokta Ranjiti.
“Bosi nimemaliza kazi”
“Safi kijana wangu, hakikisha na kesho unaifanya kazi niliyo kuagiza madhubuti”
“Sawa mkuu”
Lee Si, akakata simu akavua nguo zake zote na kuingia bafuni kuoga.
                                                                                                          ***
  Maelezo ya Shamsa, yakachukuliwa vizuri na askari wapelelezi, wakamuhoji na Sa Yoo, akaelekeza alicho kishuhudia, kisha wakaruhusiwa kuondoka kituoni. Upelelezi wa kupotea kwa mke wa daktari maarufu nchini Japan bwana Ranjiti, ukaanza mara moja, ulinzi ukaimarishwa kwenye sehemu muhimu, kama katika viwanja vya ndege, bandari na stendi zote za mabasi yaendayo nje ya mikoa.

Swala hilo likavuja kwa waandishi wa habari ambao hawakusita kutumi taaluma yao, katika kuwajulisha wananchi kwamba mke wa dokta Ranjiti amatekwa na watu wasio julikana. Picha za Phidaya zikaanza kuonyeshwa kwenye vituo mbalimbali vya televishion pamoja na kwenye magezeti yanayo toka majira ya jioni yakiwa yamekusanya habari za kutwa nzima kuanzia asubuhi hadi jioni.
Habari hizo zilizidi kuwakosesha amani Shamsa na Sa Yoo, pia walihofia usalama wao kwani hawakujua ni kitu gani kinaweza kutokea wakato wowote.

Wakarudi hotelini wakiwa katika mashaka makubwa, wakiwa wanasubiria lifti ya kupanda gorofani ifunguke, lifti ya pembeni ikafunguka, akatoka Lee Si, akionekana mwenye wasiwasi mwingi.
“Madam mu…muunataka kuniamb….ia amete…kwa?”
Lee Si, aliuliza akiwa na wasiwasi mwingi sana usoni mwake.
“Ndio mbona nilikuwa nakupigia simu hupokei?”
Sa Yoo alimuuliza Lee SSi huku akiwa amemkazia macho na kwajinsi macho yake yalivyo kuwa makubwa kiasi na makali pale anapo mkazia mtu, basi Lee Si, akajikuta akizidi kuogopa.

“Nilikuwa nimelala na simu ikawa imezima chaji”
“Mende mkubwa wewe, unajali usingizi kuliko boasi wako…..”
Sa Yoo alizungumza kwa kufoka huku akiuvuta mdomo wake, Shamsa akamzuia asimrushie kofi Lee Si, kwani alimuona hana hatia yoyote kwani kosa kubwa amelifanya Phidaya kwa kuto mtaarifu mlinzi wake huyo kwamba anatoka kama anavyo fanya siku zote. Ikabidi Lee Si, arudi nao, wakaingia kwenye lifti na kurudi hadi kwenye chumba wanacho ishi Shamsa na Sa Yoo.

Kila mmoja akakaa kwenye sehemu aliyo ona inamfaa, mawazo mengi yalizidi kumchanganya Shamsa, hakujua afanye nini ili kumkomboa mama yake.
“Wewe unakaa kimya nini sasa, toa mawazo tujue tunafanyaje”
Sa Yoo alizungumza huku kidole chake akiwa amemnyooshea Lee Si, aliye kiinamisha kichwa chake chini, Lee Si akamtazama Sa Yoo kwa macho yaliyo jaa huruma, hakuzungumza chochote zaidi ya kuangalia chini tena.
“Tusubirie tuone polisi watatuambia nini”
Shamsa alizungumza kwa sauti ya unyonge huku akimtazama Sa Yoo aliye kasirika kwa kununa.
                                                                                                  ***
   Furaha na amani ikatoweka moyoni mwa Eddy, jambo ambalo Mzee Yo alilistukia mapema, akajitahidi anampikia Eddy chakula anacho kipenda, kisha aweze kumfariji mwanaye huyo. Mzee Yo alipo maziza kupika chakula akamkaribisha Eddy mezani.

Eddy hakuzungumza chochote zaidi ya kutala taratibu, mara kadhaa alisikika akisunya, Mzee Yo akuzungumza chochote hadi walipo maliza kula chakua.
“Mbona leo una mawazo mengi?”
“Namfikiria yule nesi aliye tekwa?”
“Ahaa yule ni mke wa bwana Ranjiti, kwa jinsi ya kifo cha dokta Yan kilivyo tokea basi nahisi hapa kuna mtu anawafwatilia wafanyakazi wake”
“Una taka kuniambia yule nesi ni mke wa daktari aliye hitaji kuniua mimi?”
“Ndio”
“Hapa kuna jambo ambalo linaendelea na halieleweki?”
“Kivipi?”
“Si fahamu ila nahisi kuja kitu kinacho endelea kinacho peleka mambo yote hayo kutoke”

”Kuna haja ya kufanya uchunguzi wa chini chini”
“Basi nitaomba tuunze kuufa leo hii hii”
“Kwa leo kwako haitakuwa salama, ninaimani sasa hivi kutakuwa na msakako mkali unaendelea kwa mtu aliye mteka mke wa dokta”
“Hivi anaitwa nani?”
“Anaitwa Phidaya”
Moyo wa Eddy ukapiga paaa, akahisi labda hajalisikia vizuri jina alilo tajiwa, akamuomba Mzee Yo alitaje tena, bila hata kukosea Mzee Yo akalitaja jina hilo kama lilivyo, akazidi kumchanganya Eddy, na kumpa hisia ambazo masaa machache ya nyuma alizikataa na kuamini kwamba mke wake kwa sasa ni marehemu.

Mzee Yo majira ya jioni akaondoka mapangoni na kuelekea mjini kuchunguza ni nini kinacho endelea, huku akiwa ameagiziwa na Eddy kumnunulia nguo za Black Shadow, ili kurudi kazini kwa lengo moja kufahamu mke wa dokta Ranjiti ni Phidaya wake au laa na kama ni Phidaya wake, basi dokta huyo atatoa maelezo yakutosha juu ya kitu alicho kifanya hadi kumchukua mke wake.

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )