Sunday, May 28, 2017

SORRY MADAM -Sehemu ya 64 & 65 (Destination of my enemies)

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWAILIPOISHIA

ILIPOISHIA
Akafungua vioo vya dirishani, akachungulia chini, akashusha pumzi na kuanza kuutoa mguu wake wa kushoto kwenye sehemu ulipo kanyaga mguu wake wa kulia, lengo lake alihitaji kwenda katika dirisha linalo fwata kwa kupita katika kijinjia hicho. Phidaya alipo hakikisha kwamba ameshikilia vizuri, akaanza kutambaa kuelekea kwenye dirisha la chumba cha pili, ila kabla hajafika akajikuta akigeuka na kuangalia chini, kizunguzuku kikali kikamshika na kujikuta akipepesuka, mikono na miguu yake vikapoteza muhimili na kujikuta akianza kuelea hewani na kwenda chini kwa kasi kali, kitendo kilicho shuhudiwa na watu wengi waliopo chini, kila mmoja alishangaa kuona mwanamke huyo akianguka kutokea gorofa ya kumi kuja chini.

ENDELEA
Macho ya watu wengi yakashuhudia jinsi Phidaya anavyokuja kwa kasi chini, wakamshindikiza kwa macho yao hadi kwenye swimming poolm, lililo jaa maji liliopo chini usawa wa sehemu ambayo Phidaya aliangukia.

Vijana wawili wenye asili ya kiarabu pamoja na Rahab ambaye alikuwa ameketi pembezoni mwa swimming pool hilo akipunga upepo wakajitosa kwenye maji, kila mmoja akiwa na lengo la kwenda kumuokuoa msichana huyo. Kwa pamoja wakajikuta wakimtoa kwenye maji, kidogo Rahab akaonekana kustushwa na msichana huyo. Kutokona ni mwanamke mwenzake Rahab akaanza kumpulizia hewa, Phidaya mdomoni mwake kumpa pumzi ya ziada kutokana kuanguka kwake kumemfanya kuzimia.

Haikuchukua muda Phidaya akastuka, huku akihema, macho yake yakatua kwa Rahab aliye muinamia, akashangaa kumuona Rahab kwa maana ni mtu anye mfahamu, ila bado hakujua ni sehemu gani ambayo aliweza kumuona mwanamke huyo.
Wahuduu wa Hoteli pamoja na meneja wa hotelo hiyo wakafika baada ya kujulishwa na wateja wao kwamba kuna tukio la ajabu limetokea, katika hoteli yao, wakakuta Phidaya akiwa amefunikwa na taulo, kubwa ili kutoa ubaridi mwilini mwake na mwili nzima unamtetemeka kwa woga.

“Yupo vizuri mpeni hewa musimzunguke”
Rahab alizungumza huku akiwasogeza watu waliopo katika eneo hilo, hapakuwa na mtu aliye weza kuamini kwamba mwanamke huyo anaweza kupona, hii ni kutokana na umbali mrefu alio weza kutoka hadi chini alipo angukia.
”Mama uaitwa nani?”
Meneje alimuuliza Phidaya, aliye mtazama kwa macho makali, yalio jaa wekundu ulio sababishwa na kulia sana.
“Kwa sasa hayupo sawa, labda badae anaweza kuzungumza”
“Kuna huduma ya dharura labda tuweze kumuwahisha hospitalini.”
“Hilo pia linaweza kusaidia”

Ikaletwa gari ya wagonjwa, Phidaya akaingizwa kwenye gari, huku Rahab akiomba na yeye kwenda, akakubaliwa, kutokana na msaada wake walio weza kuufanya kwa binti huyo. Haikuwachukua muda mwingi sana wakawa wamefika hospitalini, ila kabla Phidaya hajaingizwa katika chumba cha matibabu, akamuomba Rahab kuweza kuwasiliana na mtu aliye weza kumtajia namba yake.
“Huyo ni nani?”
“Ni mlinzi wangu”
“Yupo wapi?”
“Yupo Japani”
“Anaitwa nani?”
“Lee Si”
Phidaya alipo maliza kuzungumza hayo, kitanda alicho lalia kikasukumwa ndani ya chumba hicho kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa mwili wake.

***
“Lee Si nina mazungumzo na wewe”
Shamsa alizungumza huku akiufunga mlango wa Lee Si, baada ya kuugonga kwa muda kasha ukafunguliwa. Lee Si, akavaa tisheti yake kisha na kuelekea chumbani kwa Shamsa, akamkuta akiwa amekaa na Sa Yoo wakimsubiria, sura za wasichana hao zilimuonyesha Lee Si, kwamba wana maswali mengi juu yake.

“Nimefika”
Sa Yoo, akamkata jicho Lee Si kisha akamtazama Shamsa ambaye muda wote alikuwa akifikiria jambo la kuzungumza.
“Kwa nini unatuzunguka?”
Shamsa alizungumza huku akimtazama Lee Si usoni
”Kivipi madam?”
“Tuambie madam yupo wapi, ikiwa wewe kama mlinzi wake ni lazima utatambua kuna kitu kinacho endelea, la sivyo tutakuripoti polisi na utatuambia ukweli kuhusiana na sehemu alipo mama yangu”

Lee Si, akatabasamu kwa dharau kicha akamtazama Shamsa kuanzia chini hadi juu. Dharau ya Lee Si, ikamfanya Sa Yoo, kuachia msunyo mkali, huku akilitoa na yeye jicho lake kubwa fulani kumpandisha na kumshu Lee Si juu hadi chini.
“Hata mukinipeleka polisi, munahisi nitawekwa ndani? Siku ambayo mulikwenda kununuliwa nguo mimi nilikuwepo? Kama jibu ni hapana basi tambueni kwamba sifahamu alipo madam, na mimi nikama nyinyi sote hatujui ni wapi alipo”

“Shamsa unaona dharau zake nilizo kuambia, huyu ni lazima atakuwa anafahamu”
Sa Yoo, alizungumza huku akichukua mto mdogo wa kochi na kumrushia, Lee Si, na kumbamiza nao wa uso. Lee Si, akanyanyuka kwa hasira akamfwata Sa Yoo, sehemu alipo simama, kwa lengo la kumuadhibu kwa kitendo alicho kifanya ila kabla hajamfikia, akazuiliwa na Shamsa aliye simama kwa haraka.
“Unataka kufanya nini?”

Shamsa alimuuliza kwa sauti ya msisitizo huku akimtazama Lee Si usoni mwake, Lee Si akamsukumia Shamsa pembeni, akamzaba kibao kizito Sa Yoo, aliye baki akishangaa. Kitendo hicho kikamkera sana Shamsa, akanyanyuka na kumtandika kofi zito Lee Si, aliye mtolea macho makali Shamsa, akataka kurusha ngumi, ila simu yake, ikaita, akaitoa kwa haraka mfukoni mwa suruali yake, kabla hajatazama ni nani aliye piga simu hiyo, akastukia Sa Yoo, akimpiga teke kwenye mkono alio shika simu, ikaangukia pembeni.
Lee Si akamrukia Sa Yoo kwenye kochi kabla hajampiga kofi, tayari Shamsa Alisha jiachia, na kumrukia, akamuangusha chini na kuanza kumtandika ngumi mfululizo.

Lee Si hakukubali kuona anapigwa na msichana huyo alicho kifanya ni kujigeuza, akampiga Shamsa ngumi moja aliyo izuia kwa mikono yake miwili, Sa Yoo, katika kuzungusha zungusha jicho lake, akaiona simu ya Lee Si, ikiita, hakutaka kuujali ugomvi huo alicho fanya ni kuishika simu hiyo na kuipokea.
“Haloo”
Sa Yoo, alizungumza huku akikimbilia bafuni na kuwaacha Shamsa na Lee Si wakiendelea kupigana
“Unazungumza na Rahab Praygod ninatumaini kwamba wewe ndio Lee Si”

Sa Yoo, ikabidi kuitoa simu hiyo sikioni na kuitazama namba hiyo akagundua kwamba si namba ya Japan. Akili yake ikafanya kazi haraka haraka na kujibu kwamba yeye ndio Lee Si.
“Kuna taarifa ambayo bosi wako Phidaya ameniambia nikujulishe, kwa sasa yeye yupo nchini Misri barani Afrika na yupo hospitalini kwa uchunguzi zaidi wa madaktari hii, ni baada ya kujaribu kufanya jaribio la kutaka kujiua”
Sa Yoo, akauziba mdomo wake kwa wasiwasi mwingi, akionekana kustushwa na habari hiyo.
“Alooo unanisikia?”
Rahaba alizungumza baada ya kuona mtu anaye zungumza naye amekaa kimya.

“Nakusikia, amelazwa hospitali gani?”
Rahab akalitaja jina la hospiali aliyo lazwa Phidaya, kisha akamuaga Lee Si, kutokana na kumaliza mazungumzo yake aliyo kuwa ameagizwa na Phidaya. Sa Yoo, akatoka bafuni na kurudi sebleni, akamkuta Lee Si, akiwa anavuja damu puani huku amelala sakafuni na Shamsa amesimama pembeni yake huku amekunja ngumi na kufura kwa hasira.
“Vipi?”
Sa Yoo, alimuliza Shamsa huku akiwa amemkodolea macho Lee Si, anaye jizoa zoa kunyanyuka.

“Siwezi pigana na wazembe mimi”
Shamsa alizunguza huku akiondoka karibu na Lee Si, aliye kaa kitako sakafuni akiwa haamini kwamba umahiri wake wa kupigana ameweza kuchezea kichapo ambacho hakukitarajia kabisa kutoka kwa binti huyo ambaye kwa mara ya kwanza alimchukulia binti wa kawaida.
“Nenda chumbani kwako na usije ukarudia”
Kwa haraka Sa Yoo akaituma kwa namba ya simu kwa ujumbe mfupi wa maandishi kwenye simu yake, namba ambayo ilipiga kwenye simu ya Lee Si, kisha akaifuta na kumrushia Lee Si simu yake.

“Besti hiyo puaa ilivyo kaa”
Sa Yoo alimtania Lee Si baada ya kumuona pua yake ikiwa kidogo kama imepinda, huku damu zikiendelea kumwagika. Baada ya Lee Si kutoka chumbani hapo, na Sa Yoo kuhakikisha kwa kuchungulia mlangoni kwamba Lee Si ameingia chumbani kwake akamuelezea Shamsa kila kitu alicho kizungumza kupitia simu ya Lee Si.
“Huyo mtu amesema kwamba anaitwa nani?”
“Rahab Praygod”
Jina la Rahab Praygod halikuwa ngeni masikioni mwake, ila hakuhitaji, kuliwekea maanani kwa maana majina duniani yananafanana isitoshe kwamba mtu mwenyewe aliye ipiga simu hiyo yupo nchini Misri.
“Inabidi tuondoke”
“Sawa tuanze kufwatilia maswala ya viza”
“Poa”

***
Macho ya Sabogo yaliweza kuwakumbuka Shamsa na Sa Yoo, ambao amewaona wakiwa wamesimama kwenye ofisi za shirika moja la ndege. Kutokana alisha elezwa na Black Shadow kuhusiana na binti huyo kwamba ni mwanae hakuona haja ya kuendelea kuwatazama. Akatembea kwa mwendo wa haraka hadi walipo, akamgusa Shamsa begani na kufanya Shamsa kugeuka na Sa Yoo pia kugeuka. Wote wakaonekana kumshangaa, Sabogo kwani ni jitu refu kwenda juu, na wote vimo vyao wanamfikia kiunoni.
“Ninaweza kuzungumza na nyinyi?”
Sa Yo alikubali kwa kutingisha kichwa kutokana na woga ulio mvaa gafla. Wakatoka hapo dirishani na kwenda kukaa nje ya uwanja huo wa ndege ambapo kuna mgahawa

“Naamini kwamba munanifahamu?”
“Hapana”
Sa Yoo alijibu kwa haraka sana hata kabla Shamsa kujibu.
“Mimi ni meneja wa Black Shadow ninaimani kwamba wote munamjua, ninaitwa Sabogo”
“Ahaaa wewe ndio yule ambaye ulituletea tiketi za kukaa VIP?”
“Ndio mimi haujakosea”
Furaha ikamuingia Shamsa, akaona ni bahati kubwa sana kuonana na mtu huyo kwa maana ndoto za kukutana na mpenzi wake ambaye ni Black Shadow, zinaanza kufufuka upya.

“Black Shadow yupo wapi?”
“Yupo na ninaimani pia atakuwa na furaha kuonana na nyinyi”
“Ninakuomba utupeleke sasa hivi”
Shamsa alizungumza huku akimshika, mkono Sabogo.
“Kwa mchana huu ninaimani itakuwa ni ngumu labda kwa usiku”
“Hata iwe saa nane ya usiku mimi nipo tayari kuonana naye”
“Sawa kuna sehemu nitawahitaji muje, ila hakikisheni kwamba munakuja nyinyi wawili peke yenu tu”
“Sawa”

Sabogo akaawachia namba za simu, hata wazo la kwenda Misri, barani Afrika, wakaliweka kando kwanza, moyo wa upendo juu ya Black Shadow, ukarudi kwa upya kabisa moyoni mwa Shamsa. Siku hiyo furaha ikamjaa tele moyoni mwake, hata kumbukumbu alizo ambiwa na Phidaya kwamba Black Shadow ni baba yake ziliteketea. Hakutaka kuzipa uzito wa aina yoyote kutokana anaamini kwamba Black Shadow ni mwanaume mwengine kabisa na Eddy ni mwanaume mwengine kabisa.

***
Furaha na amani ikamtoweka Madam Mery, hakujua maisha yake ya hapo mbeleni yatakuwa vipi, kwani adui yake namba moja ndio huyo amekalia kiti cha uraisi nchini Tanzania.
“Nitafanyeje?”
Ndio swali ambalo Madam Mery aliendelea kujiuliza kichwani mwake, akaendelea kuzunguka chumbani kwake, akitafakari, hakuhitaji siku hiyo kuonana na mtu wa aina yoyote hata wafanyakazi wake wa ndani. Kila alilo lifikiria alilipangua, kwani mpango wake aliona unafeli.

“Eddy, lazima nionane na Eddy ndio mtu pekee ambaye anaweza kuniunga mkono katika mpango wangu huu”
Madam Mery alizungumza huku akiifungua Laptop yake, akaanza kutafuta ni wapi alipo Eddy. Ripoti ya mwisho ambayo aliipata katika mtandao kwamba Eddy yupo Japani na nimuhalifu katika nchi hiyo anatafutwa.

Madam Mery hakuona haja ya kupoteza muda akakata tiketi kabisa kupitia mtandao, siku iliyo fwata akapanda ndege hadi Dar es Salaam, ambapo akakuta tiketi yake ikiwa tayari, akapanda ndege ya shirika la KLM na kuianza safari yake, ambayo ilimchukua masaa mengi kukaa angani.

Kitendo cha kutoka katika uwanja wa ndege akamshuhudia Shamsa akiwa na binti mmoja wakiingia kwenye gari ya kifahari na kuondoka.
Madam Mery hakuhitaji kuweka hisia za kwamba mtu aliye weza kumuona ni tofauti za Shamsa, kutokana binti huyo anamtambua vizuri sana na Alisha wahi kukaa naye na kumueleza siri nyingi kuhusiana na kikosi cha siri kinacho milikiwa na mzee Godwin baba yeka Eddy.

Madam Mery akamuomba dereva huyo kulifwata gari hilo kwa nyuma popote litakapo kwenda, dereva naye akafanya hivyo kama alivyo agizwa, gari hilo likafika kwenye moja ya hoteli mabinti hao wakashuka, Madam Mery naye akashuka na kumlipa dereva pesa yake akiamini kwamba atawakuta mapokezi Shamsa na huyo rafiki yake wa kijapani.

Hadi anaingia ndani hakuweza kuwaona, muhudumu mmoja akamkaribisha, bila kutaja haja yake, ya yeye kumfikisha hapo, ikamlazimu kuchukua chumba katika hoteli hiyo hiyo, akijipa moyo kwamba akiliona gari hilo basi Shamsa atakuwa amemuona na kama amemuona Shamsa basi Eddy hato kuwa mbali na atamueleza kila kitu kuhusiana na Tanzanani.
***
Sabogo, mara baada ya kurudi katika makao yake, kitu cha kwanza alicho kifanya akampigia simu Black Shadow na kumuomba aweze kukutana naye kwenye moja ya gorofa juu kabisa ya gorofa hilo zinazo pata gorofa, ishirini na tano.
“Kuna nini?”

“Kuna zawadi nimekuandalia”
“Sawa kaka”
Majira ya saa nne usiku, Sabogo akawa ndio mtu wa kwanza kuweza kufika katika eneo la gorofa hilo, akawaelekeza Shamsa na Sa Yoo, mara baada ya kupigiwa simu na wasichana hao. Haikuchukua muda sana Sa Yoon a Shamsa wakawa wamesha fika katika kilele cha gorofa hilo.
“Yupo wapi Black Shadow?”
Shamsa alimuliza Sabogo.
“Ninaimani kwamba yupo njiani”
Ikawalazimu wawe wavumilivu waendelee kumsubiria Black Shadow.
***
Katika kitu ambacho kilitoke kumkera na kumuudhi Lee Si ni kupigwa na Shamsa, bado hakuwa anaamini kwamba amechezea kichapo kikali kutoka kwa binti huyo. Moyoni mwake akajiapiza kuweza kumuua, iwe isiwe ni lazima awaangamize hususania cha umbea Sa Yoo. 

==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )