Saturday, May 6, 2017

Sugu: Bashite Amekataliwa na Jamii Yote, Wasanii Acheni Kutumika

Mbunge wa mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Chadema), amewataka wanasiasa kutowatumia vibaya wasanii kwa manufaa yao binafsi. Amesema Bashite ni mtu aliyekataliwa na jamii, hivyo wasanii wasikubali kutumika kumsafisha.

Ameyasema hayo jana Bungeni Mjini Dodoma alipokuwa akisoma hotuba ya kambi rasmi ya upinzani kuhusu Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo.

Aidha, Sugu amemtaka msanii ‘Roma’ kujitokeza hadharani kusema ukweli ni kipi kilichotokea na ni nani aliyehusika katika tukio hilo la utekwaji wake na wenzie.

“Wanasiasa tunatakiwa tuwaheshimu wasanii kwani ni kioo cha jamii, kuwatumia na kuwaterekeza mtakuwa hawatendei haki,”amesema Mbilinyi.

==>Msikilize Hapo Chini Akiongea


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )