Saturday, May 6, 2017

Zitto na ACT Wazalendo watuma salamu za rambirambi kufuatia vifo vya wanafunzi 32

Picha: Wajumbe wa Kamati ya Chama cha ACT Wazalendo, wakiwa wamesimama kuomboleza na kuwakumbuka wote waliopoteza maisha katika Ajali hii.

Mbunge wa Kigoma mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo Zitto Kabwe na Chama Chake cha ACT Wazalendo wametuma salamu za rambirambi kufuatia kutokea kwa ajali mbaya ya basi dogo ambalo limepelekea vifo vya wanafunzi 29, walimu 2 na dereva mmoja wa gari hiyo.

Zitto Kabwe katika salamu zake za rambirambi anasema kuwa huu ni msiba mkubwa kwa taifa.

"Moyo wangu umesinyaa baada ya kusikia Taarifa za ajali ya watoto wetu huko Karatu. Natoa salaam zangu za rambirambi kwa Wazazi wa wanafunzi wa shule ya St. Lucky na Kwa ndugu na familia za walimu na wafanyakazi wa shule waliopoteza maisha. Huu ni msiba mkubwa sana. Huzuni haielezeki. Nawaombea Kwa Mola awape wazazi na ndugu wote moyo wa subira katika mtihani huu. Ni msiba wa Taifa zima" alisema Zitto Kabwe

Katika taarifa ya Chama Cha ACT Wazalendo pia imetoa pole kwa wanafamilia, walimu

"Chama cha ACT Wazalendo kimepokea kwa majonzi na simanzi kubwa taarifa ya vifo vya wanafunzi, walimu pamoja na wafanyakazi wa Shule ya awali na msingi ya Lucky Vicent ya Jijini Arusha, vifo vilivyotokana na ajali ya basi iliyotokea katika wilaya ya Karatu mkoani Arusha. ACT Wazalendo tunatoa pole kwa wazazi waliopoteza watoto wao, ndugu na jamaa waliopoteza walimu na wafanyakazi wa shule hiyo, pamoja na watanzania wote kwa ujumla. Pia tunawaombea majeruhi wote wa ajali hii wapate kupona kwa haraka" alisema Abdallah Khamis Afisa Habari wa ACT Wazalendo
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )