Monday, June 5, 2017

Adhabu: Halima Mdee na Esther Bulaya Wapigwa Marufuku Kuhudhuria Bunge Hadi mkutano ujao wa Bunge la Bajeti ya 2018/19


Halima Mdee na Esther Bulaya wamehukumiwa kutohudhuria vikao vyote vya bunge linaloendelea mpaka mkutano ujao wa Bunge la Bajeti ya 2018/19.
 
Hukumu hiyo imeungwa mkono na wabunge wengi waliopitisha azimio hilo.
 
Mapema leo, Jumatatu Kamati ya Maadili ilisema Bulaya na Mdee wamemaliza adhabu za kawaida zilizopo kwenye kanuni za bunge.
 
Hata hivyo, Bunge liliendelea kujadili makosa ya wabunge hao wa Bunda na Kawe.
 
Mwenyekiti wa kamati hiyo, George Mkuchika aliliomba Bunge kujadili adhabu inayostahili kulingana na makosa yao.
 
Kanuni inasema, mbunge anayefanya kosa la kwanza anaweza akazuiwa kuhudhuria vikao visivyozidi 10 na atayakosea kwa mara ya pili anaweza kuzuiwa kuhudhuria vikao visivyozidi 20.


==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )