Thursday, June 8, 2017

Anna Mgwhira avuliwa uenyekiti ACT- Wazalendo

Chama cha ACT Wazalendo  kimesitisha rasmi uenyekiti wa aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho tangu kuanzishwa kwake, Anna Mghwira, baada ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro kuazia  jana  Juni 7.

Uamuzi huo umefanywa na kikao cha Kamati ya Uongozi ya chama hicho ambacho pia kimemteua Mwenyekiti wa Kamati ya Mafunzo, Oganaizesheni na Uanachama kuwa Kaimu Mwenyekiti wa chama hicho hadi uchaguzi mkuu utakapofanyika mwezi Machi mwakani.

Akitangaza uamuzi huo kwa wanahabari jana , Kaimu Kiongozi wa chama hicho, Samson Mwigamba amesema sababu kuu ya kusitisha uenyekiti wa Anna Mghwira, ni ili kumpa nafasi ya kutekeleza majukumu yake mapya aliyopewa na Rais wa Tanzania, pamoja na kumfanya asiwe na mgongano wa kimaslahi ya kichama wakati akitekeleza majumu yake kama kiongozi.

“Sisi kama ACT hatupingi uamuzi wa mamlaka ya Rais, isipokuwa kamati ya uongozi imeona ni busara kumpa nafasi Anna Mghwira kutumikia nafasi moja kama kiongozi, lakini ataendelea kuwa mwanachama wa ACT Wazalendo. Kabla ya kutangaza uamuzi huo tayari tumewasiliana naye na tumekubaliana hivyo. Tunamtakia kila la heri katika majukumu yake mapya,” alisema Ado Shaibu ambaye ni Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano kwa umma.

Pamoja na hayo Mwigamba alimpongeza  Rais kwa kuvunja miiko ya siasa za Tanzania kwa kumpatia mpinzani nafasi hiyo ndani ya serikali yake  na kuongeza kuwa kama chama hawana tatizo kwa kiongozi huyo kukabidhiwa ilani ya CCM kwa sababu anakwenda kutumikia serikali kuu na Taifa.
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )