Saturday, June 17, 2017

Makomando 7 wa Marekani wapotea baada ya meli ya kivita kugongwa Japan

Makomando saba wa kikosi cha maji cha jeshi la Marekani wameripotiwa kupotea baada ya meli yao kugongana na meli ya wafanyabiashara karibu na pwani ya Japan.

Kamanda wa meli hiyo maalum za kuwaharibu maadui inayofahamika kama USS Fitzgerald aka Destroyer, aliokolewa na kukimbizwa hospitalini kwa chopa (helicopter).

Meli hiyo iligongana na meli ya wafanyabiashara iliyokuwa na makontena umbali wa kilometa 104 Kusini-Magharibi mwa Yokosuka. Picha zilizopigwa kutoka juu zilionesha uharibifu mkubwa kwa meli hiyo kutokana na tukio hilo lililotokea majira ya saa nane na nusu usiku wa kuamkia leo, kwa muda wa Japan.

Kwa mujibu wa BBC kamanda mwingine wa meli hiyo, Cdr Bryce Benson ameokolewa na anaendelea kupata matibabu hospitalini lakini hali yake imezidi kuimarika baada ya kuhamishiwa katika hospitali ya jeshi la Marekani iliyoko Yokosuka.

Hadi kufikia majira ya asubuhi, taarifa zilizotolewa na maafisa wa jeshi la maji la Marekani zimeeleza kuwa ingawa ‘Destroyer’ ilikuwa katika hatari ya kuzama, maeneo yote ya kuingilia maji ndani ya meli hiyo tayari yameshadhibitiwa kitaalam.

==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )