Wednesday, June 21, 2017

Picha: Rais Magufuli alivyozindua Kiwanda cha TAMCO kinachounganisha Matrekta

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amezindua kiwanda cha kuunganisha matrekta cha Ursus na kiwanda cha Nondo cha Kiluwa ambapo  amewataka wawekezaji kujitokeza kwa wingi kwani Serikali iko nao bega kwa bega.

"Kiwanda ni kikubwa na kinatoa nondo ambazo zinaweza kujenga daraja lolote Tanzania au Ulaya.Tanzania tuna chuma, kwa nini tuagize chuma kutoka Brazil au China.

"Wawekezaji watafute njia ya kutumia chuma cha Tanzania badala ya kuagiza nje ya nchi  na nashauri Ajira zianze kwanza kwa vijana wa Mkoa wa Pwani'',  amesema Rais Dkt. Magufuli na kuongeza kuwa serikali inampango  wa kujenga barabara kubwa ya lami ya njia sita kutoka Dar mpaka Chalinze ambapo amewataka watanzania kuvilinda viwanda  na  amani ya Tanzania

 
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )