Wednesday, June 21, 2017

Rais Magufuli abaini uwepo wa pembejeo hewa,

Raisi John Magufuli amesema kuna pembejeo hewa  kama ilivyo kwa watumishi  na wanafunzi hewa.

Akizungumza leo (Jumatano) wakati akizindua kiwanda cha chuma cha kuunganisha matrekta cha Ursus, Rais Magufuli amesema tatizo la pembejeo hewa ni kubwa na sasa analifanyia kazi na muda wowote ataliweka hadharani.

Amesema amebaini katika mpango wa kusambaza pembejeo nchini wapo wakulima walioandikishwa majina yao lakini kumbe walishafariki zaidi ya miaka 20 iliyopita na wengine wanaodaiwa kusambaziwa kumbe hata si wakulima na hawana hata mashamba.

Rais amesema hayo katika ziara yake ya siku tatu mkoani Pwani.

Amesema tayari ameipa kazi timu maalumu ya watu kufanya uchunguzi wa kina kuhusu pembejeo hewa ambazo amedai ni nyingi na akiikamilisha ataanika hadharani madudu hayo na wahusika wote watashughulikiwa.

“Yaani hata kwenye pembejeo nimebaini zipo hewa, majina ya watu unakuta ni mtu aliyefariki miaka zaidi ya 20 iliyopita, mengine mtu hana hata shamba sasa kila kitu ilikua hewa, na hapa naamini tatizo ni kubwa lakini tutalimaliza kama lile la wanafunzi na watumishi, wapo watu wanafanya hii kazi ikikamilika tu tutaeleza,"amesema

Rais amesema asilimia 80 ya Tanzania inategemea kilimo lakini eneo hilo halina maendeleo kwa sababu wengi wanatumia jembe la mkono.

Lakini kama wakianza kutumia matrekta basi kilimo chetu nchini kitakua cha tija kwani wakulima wengi watazalisha zaidi.

Ameitaka Wizara ya viwanda na uwekezaji, wizara ya kilimo na wawekezaji wa matreta hayo waangalie suala la bei ili isiwe kubwa na kuwafanya watu kushindwa kuyanunua.

Katika ziara yake amelitaka Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) wabadiliie katika utendaji kazi sababu huko nyuma kila kilichokua kibaya akiuliza imetajwa NDC hadi akawa ameanza kutaka kufumua lakini kupitia ziara hiyo ameona mabadiliko mengi yenye tija kwenye uanzishwaji viwanda hivyo vitatu alivyotembelea Kibaha.
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )