Sunday, June 18, 2017

SORRY MADAM -Sehemu ya 70 & 71 (Destination of my enemies)

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWAILIPOISHIA
ILIPOISHIA
Eddy alipo isikia sauti ya Ranjiti kwenye simu ya raisi Praygod, akasimama kwa haraka kwenye sofa alilo kaa, kisha akaikwapua simu kutoa mkononi mwa raisi Praygod na wafanya watu wote wamshangae.
“RANJITI, SIKU NIKUKITIA MIKONONI MWANGU NITAHAKIKISHA KWAMBA KICHWA CHAKO KINAKUWA MALI YANGU”
“Wee…..weee si Eddy”
Dokta Ranjiti alizungumza kwa wasiwasi mkubwa
“NDIO MIMI NI EDDY, MUME HALALI WA PHIDAYA”
Eddy alizungumza kwa sauti yanye msisitizo na kuwafanya Rahab na raisi Praygod wote kushtuka na kujikuta wakinyanyuka kwenye sofa na kumshangaa, kwani kati yao hakuna aliye weza kumgundua kwamba kijana huyo ni Eddy, ambaye alikuwa ni waziri wa ulinzi katika serikali yao na ni adui wa mapenzi wa raisi Praygoda, kwani aliweza kugundua Eddy alishirikia tendo la ndoa na mke wake kipenzi Rahab.

ENDELEA
   Simu ikakatwa na kumfanya Eddy kuishusha simu hiyo kutoka sikioni mwake kwa hasira. Hakuhitaji kuujali mshangao wa Rahab na raisi Praygod kwa maana alitambua ya kwamba ni lazima watapata mshangao huo ndio maana hakuhitaji sauti yake iweze kusikika kwa Rahab na mumewe.
“Eddy ni wewe?”
Raisi Praygod alizungumza huku akiendela kumshangaa Eddy aliyesimama, akionekana ni mwingi wa hasira.
“Hilo ni jibu na si swali”

Eddy alizungumza huku akimrudishia simu raisi Praygod. Eddy akamtazama Sa Yoo, na kumpa ishara ya kunyanyuka ili waondoke.
“Ahaa hapana Eddy, tukae tuzungumze”
Raisi Praygod alizungumza kwa busara sana, huku akimtazama Eddy machoni.
“Nikae wakati sifahamu mke wangu ni wapi alipo”
“Ndio maan mke wangu alimfwata huyo binti akimini ya kwamba yupo peke yake na alihitaji anahakikisha kwamba anamkomboa mkeo”
“Eddy, natambua haupo vizuri, hembu kaa basi tuangalie ni nini cha kufanya kwa wakati huu, ili kumuokoa Phidaya”
“Eddy kaa”

Sa Yoo alizungumza kwa sauti ya upole. Taratibu Eddy akakaa sehemu ambayo alikuwa amekaa kwa mara ya kwanza.
“Ila ninawazo moja. Munaonaje tukaifwatilia simu hiyo kupitia satelaiti”
Sa Yoo alizungumza huku akiwatazama watu wote, Rahab akanyanyuka na kuwaomba wamsubirie. Akaingia chumbani kwake, alipo toka akarudi akiwa amebeba laptop aina ya Apple(macbook air), huku mkono wake mwingine akiwa ameshika karatasi mbili ndogo.

“Kuna namba za simu yangu ile nilizo zinunua, hizi hapa”
Sa Yoo akanyanyuka na kusogea sehemu alipo Rahab, akachukua karatasi hizo na kuzitazama vizuri, akaiziona namba ambazo zimesajiliwa simu hiyo na hata endapo itakuwa imezimwa, kwa kupitia sateleitii ni lazima utaipata. Kwa haraka Sa Yoo akaanza kuifanya kazi hiyo kutokana ana ujuzi wa kazi hiyo.

Kila mtu macho yake akayaweka kwenye kioo cha Laptop hiyo, inayo tafuta kwa kasi ni wapi ilipo simu ya Rahab. Ndani ya sekunde arobaini na moja, tayari ramani ikaanza kujitokeza kwenye lapotop, alama ya kijana ikaanza kujionyesha kwenye ramani hiyo ikiashiria kwamba ndipo sehemu ilipo simu hiyo.

“Hii simu ipo katika mtaa El khaing, na sisi tupo huku Al Kerdas. Ili kuweza kufika sehemu naamini ilipo kambi hiyo ni lazima kupita katika daraja la Qasr al-nil ili kuweza kufika. Na kwa haraka haraka tunaweza kuchukua muda kama lisaa moja na nusu hivi”
Sa Yoo alizungumza huku akiwaonyesha kwa kidole jinsi ramani hiyo inavyo kwenda.
“Ila simu yangu nahisi kama niliipoteza walivyo nitelekeza”
“Ulirudije huku?”
Sa Yoo alimuuliza Rahab huku akiwa amemtumbulia macho
“Nilirudi kwa kukimbia, kutokana huo mtaa walio niacha niliweza kuufahamu kwani ni kwa mara kadhaa ni kichukua mazoezi asubuhi huwa ninapita hapo”

“Ulilipita hili daraja?”
Ikambidi Rahab kuitazama vizuri ramani hiyo.
“Hapana sikupita”
“Basi, inabidi kuweza kuifwatilia simu hii sehmu ilipo”
Sa Yoo alizidi kuzungumza kwa kujiamini na kwa msisitizo mkubwa.
“Sa Yoo unaweza kuitafuta namba ya huyo Ranjiti sehemu ilipo tokea”
“Yaa ngoja mara moja”
Sa Yoo akaaiombanamba hiyo na kuonyeshwa na raisi Praygod, ndani ya dakika moja akafanikiwa kujua ni wapi namba hiyo inapotokea.

“Sehemu ni ile ile kama nilivyo sema”
Sa Yoo alizungumza kwa msisitizo huku akiwaonyesha sehemu alama ya simu hiyo inapo onekana.
“Inabidi twende muda huu huu”
Raisi Praygod alishauri, hapakuwa na mtu aliye weza kupinga swala hilo, wakatoka wote huku Sa Yoo akiwa ameibeba laptop. Wakaingia kwenye gari, na Rahab akawa dereva wa safari hiyo.
                                                                                                                    ***
Dokta Ranjiti akakata simu huku mwili mzima ukiwa unamtetemeka, akahisi kitu alicho kisikia labda inaweza kuwa ni ndoto. Adrus akabaki akimtumbuli macho bosi wake huyo asijue ni kitu gani ambacho amezungumza na mtu aliye mpigia simu.
“Bosi”
Adrus aliita, ila dokta Ranjiti hakuzungumza chochote zaidi ya kubaki akimtazama, Adrus aliye jawa na shauku ya kuhitaji kujua ni kitu gani ambacho kimetoka.

“Bosi kuna kitu gani kilicho endelea?”
“Amepokea EDDY”
“Eddy ndio nani?”
Dokta Ranjiti hakujibu kitu chochote zaidi ya kunyanyuka kwenye kiti alicho kalia, akatoka ofisini kwake pasipo kulijibu swali la Adrus, moja kwa moja akaelekea chumbani alipo muacha Phiday, akamkuta akitoka bafuni kuoga.
“Vaa vaaa nguo tunaondoka”
Dokta Ranjiti alizungumza huku jasho likimwagika, mwili mzima. Phidaya akagundua kwamba kuna tatizo ambalo limetokea kwa Ranjiti.

“Tnakwenda wapi?”
“Kwani hapa ni kwako. Vaa tuondoke sasa hivi”
Ikambidi dokta Ranjiti aanze kutafuta nguo za Phidaya alizokuwa amezitupa chini, kipindi akimlazimisha kufanya tendo la ndoa.
“Vaa vaaa…mama”
Ranjiti akaendelea kumsisitiza Phidaya, ambaye akaanza kuvaa huku kichwani mwake akijiuliza ni nini kinacho endelea. Alipo maliza kuvaa nguo zake, dokta Ranjiti akamshika mkono na wote wawili wakatoka kwenye chumba hicho na moja kwa moja dokta Ranjiti akaelekea sehemu kulipo na gari lake.

“Adrus ingia ndani ya gari munisindikize bandarini”
“Sawa mkuu”
Adrus akaingia ndani ya gari, akawasha gari hilo aina ya BMW X5. Wakati wote huo Phidaya, alikaa kimya, ila moyoni mwake akawa anaomba Mungu amsaidie lolote liweze kutokea, ila si kuendelea kukaa mikononi mwa Ranjiti. Wakaondoka eneo la ngome yao kwa mwendo wa kasi hadi walinzi wengine wakabaki wakishangaa.
                                                                                                               ***
Madam Mery baada ya kuamka moja kwa moja akaelekea chumbani kwa Eddy kutazama kama yupo, ila hakumkuta. Hakuwa na wasiwasi wowote zaidi ya kuamua kueleka katika chumba wanapo lala Shamsa na Sa Yo, akaugonga mlango mara tatu, hakusikia kitu chochote, alicho kifanya ni kuusukuma mlango huo na kuukuta upo wazi, akaingia ndani na kumkuta Shamsa akiwa amelala kitandani.

Akamsogelea huku akimuita jina lake, ila Shamsa hakuitika. Akafika kitandani na kuanza kumtingisha, ila Shamsa hakuitika, kitu kilicho anza kumpa wasiwasi madam Mery. Akajaribu kumpima mapigo yake ya moyo na kukuta yakiwa hayafanyi kazi.

“Mungu wangu”
Madam Mery alistuka, kiasi cha kuanza kutokwa na kijasho chembamba usoni mwake.
“SHAMSA, SHAMSA, SHAMSA”
Madam Mery akajaribu kumtingisha tena, ila Shamsa hakujibu chochote, Madam Mery kwa haraka akanyanyuka kitandani hapo, kwa haraka akafungua mlango wa bafuni na kuchungulia kama Sa Yoo atakuwepo, ila hakukuta
mtu.

“Sa Yoo, Sa Yoo”
Madam Mery kwa kuchanganyikiwa, alijikuta akiita huku akimtafuta Sa Yoo hadi ndani ya kabati la kuhifadhia nguo. Hakumkuta mtu, wazo la kuomba msaada katika uongozi wa hoteli hiyo ukamjia kichwani, akataka kukimbia na kutoka nje, ili kwenda kuwaita, ila akahisi kwamba atachelewa zaidi, akaisogelea simu iliyopo mezani na kuminya namba za wahudumu.
“Nahitaji msaada”
Madam Mery alizungumza kwa sauti iliyo jaa wasiwasi mwingi, muhudumu akauliza ni chumba namba, ngapi. Akamtajia namba ya chumba.  Hazikupita dakika tatu wahudumu wawili wa kike walio valia sare zilizo wakaa vizuri mwilini mwao, wakaingia ndani ya chumba hicho.

“Mwanangu hapa anatatizo”
Madam Mery alizungumza huku akiwaonyesha wahudumu hao sehemu alipo Shamsa. Wahudumu hao, wakamsogela Shamsa, wakajaribu kumtingisha, kila mmoja wasiwasi ukamuingia kwani Shamsa hakujibu chochote. Muhudumu mmoja akajaribu kumpima kama ana pumua, ila jibu alilo lipata ni sawa na jibu alilo lipata Madam Mery.

“Piga simu kitengo cha dharura”
Muhudumu huyo alimuambia muhudumu mwenzake, kwa haraka akatoa simu zao maalumu wanazo zitumia wakiwa kazini, akapiga simu kwenye kitengo cha dharura kilichopo hapo hotelini. Muhudumu akaelezea tatizo lililomo ndani ya chumbu hicho.
“Tunakuja”
Sauti nzito ya kiume ilizungumza, na simu ikakatwa.
“Amefanya nini huyu?”

Muhudumu mmoja alimuuliza Madam Mery, ambaye macho yote yalisha anza kutwaliwa na wekundu na machozi kwa mbali yalisha anza kumwagika.
“Mimi sifahamu nimekuja kuwatembela asubuhi, wezake hawapo nay eye nimemkuta hapo kalala, nimemuita ila hakujibu chochote.”
“Mwenzake ameenda wapi?”
Kabla madam Mery hajajibu chochote, mlango ukafunguliwa, wakaingia wanaume watatu huku wote wakiwa wamevalia makoti meupe, mmoja wao akiwa amevalia kipimo cha kupimia mapigo ya moyo shingoni mwake. Kwa haraka haraka Madam Mery akatambu kwamba hao watakuwa ni madaktari.

“Mgonjwa yupo  wapi?”
Dokta aliye valia kipimo hicho alizungumza, muhudumu mmoja akamuonyesha kwa kidole. Pasipo kupoteza muda daktari huyo akaanza kumpima Shamsa kifuani mwake. Madam Mery alipo yatupia macho yake usoni mwa dokta huyo akagundua kwamba kuna tatizo, kwa maana sura ya daktari, ilanza kubadiliika kila alipo jaribu kukihamisha hamisha kipimo chake kifuani mwa Shamsa.
                                                                                                       ***
“Ngoja ngoja mara moja”
Sa Yoo alizungumza huku macho yakiwa yametoka akiitazama laptop. Alama inayo onyesha simu ya dokta Ranjiti lianza kutembea. Kitu kilicho ashiria kwamba dokta huyo anaondoka katika sehemu alipo kuwepo.
“Kuna nini?”
Rahab aliuliza huku akipunguza mwendo kasi wa gari.
“Anaondoka katika eneo alilo kuwepo”
Sa Yoo aliye kaa siti ya nyuma na Eddy alimuonyesha Eddy kwa kidole.

“Hembu nione”
Rahab alizungumza na kumfanya Sa Yoo kumpa laptop, hiyo. Rahab akasimamisha gari pembani na kuanza kuangalia ramani hiyo. Akashuhudia jinsi alama hiyo inavyo tembea kwa kasi kueleka upande mwingine ambao si ule ambao wanao tokea.
“Honye hembu naomba umpishe Sa Yoo akae hapa mbele”
Raisi Praygod hakubisha, Sa Yoo akapita katikati ya siti baada ya raisi Praygod kushuka, kisha akaka mbele na kuichukua laptop hiyo.
“Naamini unatambua kazi ambayo imekuweka hapa mbele”
“Ndio, twende”

Rahab akawasha gari na kuanza kuondoka kwa mwendo wa kasi kiasi, kila muda ulivyo zidi kwenda ndivyo jinsi alivyo zidi kuongeza mwendo kasi wa gari. Sa Yoo kazi yake ikawa ni kumpa maelekezo ya kuweza kukunja katika njia za vichochoro zinavyo onekanana kwenye ramani hiyo ili kuweza kuiwahi gari hiyo.
“Tunaikaribia, ipo kama kilomita moja mbele”
“Usijali”
Kwa muda wote huo, Eddy hakuzungumza kitu cha aina yoyote, akilini mwake akawa anafikiria ni adhabu gani ambayo anaweza kumpatia dokta Ranjiti pale tu atakapo mtia mikononi mwake.

Picha ya jinsi Phidaya akiingiliwa kimwili na dokta Ranjiti ikaanza kumjia kichwani mwake, jambo lililo mfanya hasira yake izidi kumpanda. Raisi Praygod, mara kwa mara akawa anamtazama Eddy kwa jicho la kuiba, akaweza kugundua hasira aliyo kuwa nayo Eddy, kwa maana kwa mara kadhaa, aliweza kuona jinsi kifua chake, kinavyo panda na kushuka kwa kuhema kwa nguvu. Breki za gafla alizo zifunga Rahab, zikamstua Eddy na kumtoa kwenye dibwi la mawazo mabaya aliyo kuwa nayo.

“Fala kweli huyu”
Rahab alizungumza huku akiminya honi, akimpigia dereva wa gari ndogo aliye simama gafla barabarani kwa lengo la kugeuza, pasipo kuonyesha ishara yoyote.
“Pita huko pembeni”
Raisi Praygod alimshauri, Rahab akafanya hivyo, uzuri ni kwamba Rahab, katika swala zima la uendeshaji wa gari yupo makini sana na ni mtaalamu wa kufanya hivyo. Alipo hakikisha gari limekaa sawa barabarani, akaendelea kuongez amwendo kasi wa gari hilo.


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )