Sunday, June 25, 2017

SORRY MADAM -Sehemu ya 72 & 73 (Destination of my enemies)

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWAILIPOISHIA
ILIPOISHIA
Nusu saa zima likakatiaza, Shamsa mapigo yake ya moyo hayakuweza kurudi, kila daktari aliye kuwemo kwenye chumba hicho akakata tamaa. Hadi daktari mkuu Bi. Sharmaa.
“Dokta mgonjwa ameshafariki huyu”
Daktari msaidizi alizungumza kwa msisitizo.
“Muandaeni kwa ajili ya kumpeleka Mochwari”
Bi Sharmaa alizungumza huku machozi yakimlenga lenga. Kwa kipindi cha miaka ishirini katika kazi yake ya udaktari hakuna siku ambayo aliweza kuguswa na kifo cha mgonjwa, kama kifo cha Shamsa. Hakuhitaji kulia mbele za watu, akafungua mlango na kutoka
“Dokta hali ya mgonjwa vipi?”
Madam Mery alimuuliza Bi Sharmaa, huku akimtazama mwana mama huyo. Bi Sharmaa, akamtazama madam Mery kwa macho yaliyo jaa huruma, mbaya zaidi machozi akajikuta yakimwagika. Kitu kilichomfanya madam Mery kuhisi hali ya hatari imetoke
“SHAMSA AMEFARIKI DUNIA. SAMAHANI KWA HILO”
Bi Sharmaa alizungumza na kuondoka na kumuacha Madam Mery akiwa mdomo wazi asijue afanye nini.

ENDELEA
Taratibu Madam Mery akajikuta akitafuta sehemu na kukaa, mwili mzima ulimuishia nguvu, kifo cha Shamsa ni kifo kilicho mstaajabisha kwa maana ni jana mchana alikuwa naye kutwa nzima.
‘Sasa nitafanyaje mimi?’
Ni swali alilio jiuliza madam Mery akiendelea kububujikwa na machozi usoni mwake
                                                                                                       ***
Safari ya kufika katika nyumba ya raisi Praygod haikuchukua muda sana, kila mtu ndani ya gari hakuzungumza chochote, kila mtu kichwani mwake aliwaza chake. Rahab akaonekana kustuka baada ya kuukuta mlango wa kuingilia ukiwa na tofauti kidogo na jinsi walivyo uacha.

“Vipi”
Raisi Praygod aliuliza baada ya kuona mabadiliko ya sura ya Rahab.
“Kuna tatizo ndani, nisubirini nje”
Rahab alizungumza kwa kujiamini na kuwaacha Sa Yoo na Raisi Praygod kusimama. Eddy akaarudi hatua mbili nyuma kutoka katika sehemu alipo simama na kutazama upande wa pili wa nyumba ambapo aliweza kuona mlango wa sehemu hiyo ya nyuma ukiwa wazi.

Bila kumueleza mtu yoyote kitu, akaanza kuelekea kwenye mlango huo kwa tahadhari kubwa.  Kitendo cha kufika karibu na mlango huo, kufumba na kufumbua, akastukia gongo zito likitua kifuani mwake na kumuangusha chini. Akiwa amelala chini akastukia mtu akiwa amesimama mbele yake, cha kushangaza Eddy akajikuta akiishiwa nguvu na kubaki akimtumbulia macho mtu huyo.
                                                                                                      ***
   Phidaya baada ya kuingia ndani ya Taksi moja kwa moja akamuomba dereva taksi ampeleke nyumbani kwa raisi Praygod. Hawakuchukua muda mwingi wakafanikiwa kufika nyumbani kwa raisi Praygod. Hali ya ukimya ikaanza kumpa wasiwasi mwingi Phidaya, kwani tangu akae wiki kadhaa kwenye nyumba hiyo hajawahi kuona ukimya wa namna hiyo. Hapakuwa na sauti ya Tv au redio kama ilivyo zoeleka. Kwa haraka akaangaza macho yake huku na kule, hakuliona gari la Raisi Praygod analo litumia.

‘Wamekwenda wapi?’
Ni swali ambalo Phidaya alijiuliza baada ya kuufungua mlango, huku akiwa na mashaka moyoni mwake. Akaanza kuingia ndani akiwa katika mwendo wa tahadari, kama alivyo fikiria kichwani mwake kweli hakukuta mtu wa aina yoyote ndani humo.
Akiwa katika kushangaa shangaa, akastukia mlango ukifunguliwa, akageuka kwa haraka na kumkuta dereva taksi aliye mleta eneo hilo akiwa amesimama, uso wake ukionekana ukiwa katika hali ya hasira tofauti na jinsi alivyo muacha ndani ya gari.

“Unanichelewesha dada nahitaji pesa yangu”
Dereva taksi alizungumza kwa msisitizo mkubwa, ulio mfanya Phidaya kuingiwa na hofu kidogo. Dereva huyo anaye onekana ni mzee wa makamu kiasi mwenye ndevu nyingi usono mwake, zilizo fungamana kama ndevu za gaidi mmoja aliye kuwaa maarufu duniani kwa usumbufu wake, Osama Bin Laden. Mavazi aliyo yavaa yalidhihirisha kwamba ni mtu wa sala na asiye penda ujinga katika mambo yake.
“Ku….kuu kuna ndugu zangu na…wasu….biri waniletee pesa”
“Hadi saa ngapi, nimekaa hapo nje na kusubiria au unaniletea utapeli wako si ndio?”

Mzee huyo alizidi kumjia juu Phidaya na kumfanya azidi kuchanganyikiwa kwa woga. Dereva huyo akazidi kuikunja sura yake huku akianza kumsogelea taratibu Phidaya, ambaye naye alianza kurudi nyuma kwa woga. Macho ya mzee huyo yakaanza kumtazama Phidaya kuanzia juu hadi chini, taratibu macho ya mzeee huyo yakaanza kumlegea na kuingia na tamaa ya mapenzi, alipo dhibitisha kwamba hakuna mtu mwengine yoyote ndani ya nyumba hiyo dhaidi ya wao wawili tu.

“Naomba pesa yanguuu”
Mzee huyo alizungumza huku macho yakimlegea, sehemu ya mbele ya suruali yake maeneo ya zipu, ikaanza kutuna taratibu, kitu kilicho mpa Phidaya ufafanuzi wa kwanini mzee huyo aliingia humo ndani, ingali alisha mueleza amsubirie kwenye gari. Phidaya katika kurudi rudi kwake nyuma akafanikiwa kufika kwenye mlango wa kutokea nje upande wa pili wa nyumba hiyo. Mzee huyo bila hata kusita akaanza kumkimbiza Phidaya, bila ya kujali nini hatari ya yeye kufanya hivyo.

Akilini mwake tayari alisha tawaliwa na jini la mahaba na alicho kihitaji yeye kwa wakati huo ni penzi la Phidaya mwanamke aliye muona ni mzuri kuliko hata wake zake wanne alio waacha nyumbani kwake. Phidaya akafanikiwa kutoka nje na kumuacha mzee huyo hatua kadhaa, kwa haraka Phidaya  akatazama tazama eneo la nyuma ya nyumba hiyo, kulipo hifadhiwa, baadhi ya vitu vilivyo malizia ujenzi wa nyumba hiyo.

Kwa haraka Phidaya akaokota moja ya gongo na kulishika kwa umakini kitendo cha mzee huyo kutokeza sura yake kwenye kona aliyo jibanza Phidaya, gongo zito  likatua kwenye pua yake, kitendo kilicho mfanya mzee huyo kutoa ukelele mkali wa maumivu. Phidaya akamuongeza mzee huyo gongo jengine la mgongo na kumfanya mzee huyo kutoka baru,  moja kwa moja akaelekea kwenye gari lake na kuondoka eneo hilo akiyasikiulizia maumivu makali ya mgongo aliyo yapata.

Phidaya akashusha pumzi nyingi huku taratibu akikaa chini, machozi yakimwagika usoni mwake. Kwa msongamano wa mawazo na kuchoka, usingizi ukaanza kumnyemelea Phidaya taratibu na kujikuta akipitiwa na usingizi akiwa amekaa eneo hilo huku gongo lake akiwa amelishika mkononi. Haukupita muda mlio wa gari ukamstua na kujikuta akikurupuka na kusimama huku mapigo yake ya moyo yakimuenda kasi.

Akajibanza tena kwenye kona yake, kitendo cha kuchungulia, akamuona mwanaume aliye kuwa akimkimbiaza amesimama katika eneo la nyumba hiyo, kwa bahati mbaya Phidaya katika kurudi nyuma akajikuta akikanyaga kipande cha bati, kilicho toa ukelele ulio mstua mtu aliye kuwa akimkimbiza. Phidaya  mwili mzima ukamtetemeka baada ya kumuona mtu huyo akitazama eneo hilo kwa umakini na kuanza kutembea hatua za tahadari akimfwata.

Phidaya huku akiwa anatetemeka mwili mzima akalishika vizuri gongo lake, kwa mikono miwili, mtu huyo aliye hisi amumuona akazidi kumfwata , kabla hajaufikia mlango, Phidaya akalirusha gongo hilo lililo tua kifuani mwa mtu huyo na kumuangusha chini. Kwa haraka Phidaya akajitokeza  mbele ya mtu huyo kwa haraka akihitaji kuliokota gongo lake. Mtu huyo alionekana kuzubaa akimshangaa.

Phidaya bila kupoteza muda akaliokota gongo lake, baada ya kumuona mtu huyo akiwa anamshangaa shangaa pasipo kufanya kitu chochote. Akalivuta kwa nguvu na kutaka kulishusha kichwani mwa mtu huyo anaye muona ni miongoni mwa watu walio agizwa na dokta Ranjiti.

“Phidaya Stop”(Phidaya acha)
Sauti ya mwanaume huyo ikamfanya Phidaya kusita kidogo, kwani si sauti ngeni kwenye masikio yake.
“Phidaya ni mimi Eddy”
Phidaya akajikta kigugumizi kikali kikimshika, huku kikiambatana na bumbuazi kali.
“Tafadhali Phidaya ni muda mrefu nilikuwa nikikitafuta mke wangu, tafadhali usinidhuru”

Eddy alizungumza huku taratibu akinyanyuka, akampeleka Phidaya mkono wa kulia huku akihitaji kumshika ila Phidaya akaukataa mkono huo, kwani sauti ndio ni ya mume wake Eddu ila sura ndio inayo mzuzua.
Phidaya akalivuta gongo lake kwa nguvu na kutaka kumpiga nalo Eddy, akiamini mtu huyo anatumia sauti ya mume wake Eddy.
“PHIDAYAAAA”
Sauti ya Rahab ndio iliyo mfanya Phidaya kusita kwa mara nyingine, huku sura yake akimtazama Rahab aliye tokea kwenye mlango uliopo eneo hilo. Sauti ya Rahab iliwastua Sa Yoo na raisi Praygod na wote kwa pamoja wakakimbilia eneo la nyuma ya nyumba hiyo inapo tokea sauti hiyo.

Wote wakamkuta Phidaya akiwa amelishikilia gongo lake kwa mikono miwili huku mwili mzima ukimtetemeka kwa hasira.
“Madam”
Sa Yoo aliita huku macho yakiwa yamemtoka.
“Madam ni mimi Sa Yoo”
Sa Yoo alizungumza huku akimsogelea Phidaya. Kila mtu alikaa kimya akiwatazama Phidaya na Sa Yoo
“Upo katika mikono salama, madam”
“Shamsa yupo wapi?”
Phidaya alizungumza akiwa bado hajalishusha gongo lake analo taka kumpiga nalo Eddy asiye muamini kama ni Eddy kweli.

“Shasma nimemuacha hotelini, naamini tukitoka hapa tutakwenda kumuona”
Kwa maneno ya Sa Yoo, kidogo Phidaya akaanza kiliteremsha gongo lake chini, Sa Yoo akalichukua gongo hilo na kulitupa pembeni kisha akakumbatiana na Phidaya, wote wakajikuta wakimwagikwa na machozi.
“Nahitaji kuonana na Shamsa anidhibitishie kwamba huyu ni Eddy au laa”
“Sawa hakuna tatizo ila ninaomba uamini kwamba huyo ndio mumeo. Ila hiyo ni sura bandia aliyo ivaa alifanyiwa oparesheni akiwa Japani”

“Sitaki kuliamini hilo nahitaji kuonana na Shamsa mwanangu kwanza”
Hapakuwa na mtu aliye weza kubisha hilo. Wala Eddy hakuzungumza chochote zaidi ya moyoni mwake kujawa na furaha ya kuiweza kumuona mke wake. Hapakuwa na haja ya kuingia ndani wote wakaingia kwenye gari. Safari ya hotelini ikaanza, kwa mara kadhaa, Phidaya aligeuka nyuma kumtazama Eddy, ila moyoni mwake hakuhitaji kukubali kwamba huyo ni mumewe.

    Wakafika hotelini na wote wakashuka, moja kwa moja wakelekea kwenye chumba ambacho analala Shamsa na Sa Yoo. Wakaingia kwenye chumba  ila hawakumkuta Shamsa.
“Anaweza kuwa katika chumba cha madam Mery”
Sa Yoo alizungumza nakutoka kuelekea kwenye chumba hicho ila hakumkuta pia madama Mery, hakuwa na mashaka yoyote akaamini kwamba Shamsa na madama Mery wanaweza kuwa pamoja. Akatoka kwenye chumba hicho na kuanza kutembea kwa hatua za haraka kurudi katika chumba alipo waacha wezake, kabla hajakifikia akakutana na muhudumu, akamsimamisha.

“Samahani dada, kuna mwenzangu yule mwenye asili ya kiarabu arabu umemuona wapi?”
“Wa chumba kipi?”
“Ninalala naye chumba hicho hapo”
Sa Yoo akamuonyesha muhudumu huyo kwa kutumia mkono, muhudumnu akageuka nyuma, akakitazama chumba anacho onyeshwa na Sa Yoo, akashusha pumzi nyingi kisha akamgeukia Sa Yoo na kumtazama usoni. 

Advertisement
tang
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )