Loading...

Wednesday, June 21, 2017

Urusi Yaitimua Ndege ya NATO Iliyokuwa Ikimfukuzia Waziri wake wa Ulinzi

Ndege ya kijeshi ya Urusi, Su-27 imefanikiwa kuitimua ndege ya jeshi la NATO, F16   ambayo ilikuwa ikiifukuzia ndege aliyokuwa amepanda waziri wa Ulinzi wa Urusi, Sergei Shoigu

Vyombo vya habari  Urusi vimesema  kuwa tukio hilo limetokea  katika anga ya kimataifa eneo la Baltic, wakati Sergei Shoigu alikuwa akisafiri kuenda himaya ya Urusi ya Kaliningrad.

NATO  baadaye ilisema ilifuatilia ndege hiyo kwa kuwa haikujitambulisha.

Kwa mujibu wa  mashirika ya habari ya Urusi ndege ya F16 ilipita karibu na ndege ya Waziri wa Ulinzi, Shoigu, kisha ndege ya Urusi ya Su-27, ikaingilia kati na kutoa ishara kuonyesha kuwa ilikuwa imejihami, kisha ndege ya Nato ikaondoka.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )