Wednesday, June 28, 2017

Zitto Kabwe Avunja Ukimya Mauaji Kibiti


Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe amesema suala la mauaji yanayoendelea katika wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji, linahitaji mshikamano na kuwa mauaji hayo hayapewi nafasi ya kuendelea.

Zitto ameandika hayo leo (Jumatano) kwenye ukurasa wake wa  facebook na twitter na kutaka taifa lizungumze lugha moja ili kukabiliana na mauaji hayo.

“Ninarejea wito nilioutoa siku zilizopita kuwa ninatarajia Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama itakwenda eneo la MKIRU kuzungumza na wananchi wa kule ili kupata maarifa ya mbinu za kuishauri na kuisimamia Serikali kudhibiti mambo na kuimarisha usalama.” Ameandika Zitto.

Advertisement
tang
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )