Friday, July 7, 2017

Hakimu mwingine anayesikiliza ya Lema ajitoa

Hakimu Patricia Kisinda aliyekuwa akisikiliza kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Godbless Lema dhidi ya Rais Dkt Magufuli amejitoa baada ya upande wa Jamhuri kusema kuwa hawana imani naye.

Wakili wa Serikali Sabina Silayo alisema kuwa hawawezi kusoma hoja za awali za kesi hiyo kwani hawana imani na  hakimu huyo kutokana na kuwa na urafiki na mke wa mtuhumiwa, Godbless Lema jambo ambalo linaweza kuathiri mwenendo wa kesi na haki isitendeke.

Licha ya kuwa upande wa utetezi ulilipinga hilo wakisema kuwa haina uzito na kwamba watanzania wote ni marafiki na ndugu, lakini hakimu huyo aliridhia kujiondoa katika kesi hiyo ambayo inatarajiwa kuendelea tena Agosti 8 mwaka huu ambapo hoja za awali zitasomwa huku jalada likipelekwa kwa Hakimu Mfawidhi ili apangiwe hakimu mwingine.

Hakimu huyo ni wa pili kujitoa katika kesi hiyo, kwani Mei 29, Hakimu Mkazi wa Mkoa wa  Arusha, Desderi Kamugisha pia alijitoa kwa maelezo kuwa hawezi kusikiliza kesi zote nne zinazomkabili Lema  hivyo kuwaeleza mahakimu wengine watapangiwa kesi hiyo.

Wakili wa Lema, Shedrack Mfinanga aliiomba mahakama kuahirisha kesi hiyo kutokana na mteja wake kutokuwapo mahakamani kwani anaumwa.
Advertisement
tang
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )