Monday, July 10, 2017

Mkapa: Takwimu Zitawasaida kupunguza Upumbavu Wale Niliowaita Hivyo Wakati wa Kampeni

Rais Mstaafu awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa amefunguka na kusema tafiti zilizotolewa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Ally Mwalimu zitawafungua kidogo wale watu aliowaita wapumbavu kipindi cha kampeni za uchaguzi

Mhe. Mkapa amesema hayo leo alipokuwa wilayani Chato mkoani Geita wakati akikabidhi nyumba 50 zilizojengwa na taasisi yake The Benjamin William Mkapa Foundation (BMF)na kusema kwa takwimu mbalimbali zilizotolewa na waziri kwa upande wa sekta ya afya tu kunatosha kuwapunguza upumbavu watu aliowahi kuwaita wapumbavu ambao ni wapinzani.

"Kwa takwimu alizotoa Waziri wa Afya juu ya maendeleo ya afya nchini na mipango ya afya tu, naamini itapunguza kidogo 'Upumbavu' wa wale niliowahi kuwaita wapumbavu siku za nyuma" alisema Mkapa

Mbali na hilo Rais mtaafu alieleza sababu kadhaa zilizomfanya kumteua kwa mara ya kwanza John Pombe Magufuli kuwa Naibu Waziri na baadaye kumteua kuwa Waziri kabisaa kuwa ni pamoja na uchapaji kazi wake

"Mimi nilimteua Magufuli kuwa Naibu Waziri na baadaye kuwa waziri kutokana na utandaji wake wa kazi, nguvu zake na hali yake ya kufanya kazi, kwani alikuwa ni mtu mwenye upendo wa dhati na kujali kile anachokifanya" alisema Rais Mstaafu Benjamin Mkapa

Aidha Mkapa alisema yeye ni Rais mstaafu lakini hajastaafu kukitumikia chama chake Chama Cha Mapinduzi na kusema hawezi kuja kuondoka ndani ya CCM mpaka siku malaika wa mbinguni watakapokuja kumchukua.

"Mimi sijastaafu mapenzi ndani ya Chama changu cha CCM, nitaendelea kukitumikia chama changu mpaka siku Mungu atakaponiita, ndiyo nitaacha kukutumikia chama" alisema Benjamin Mkapa

Rais Mstaafum Benjamin Mkapa mwaka 2015 katika uzinduzi wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi aliwasema kuwa watu wanaojiita ni chama cha ukombozi ni wapumbavu kwani Tanzania tayari ilishakombolewa na ASP na TANU
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )