Tuesday, July 4, 2017

Mwanamke amwaga machozi mbele ya Rais Magufuli Mwanza

Rais John Magufuli amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela kuyafanyia kazi malalamiko ya mwanamke mmoja mkazi wa Sengerema aliyedai kunyanyaswa na kuvunjiwa nyumba yake.

Rais ametoa agizo hilo leo (Jumanne Julai 4) wakati akizindua mradi wa maji, wilayani Sengerema na kumtaka Mongela kuchukua namba ya simu ya mwanamke huyo aliyejitambulisha kwa jina la Rosemary Simon, ili atatuliwe tatizo lake.

 Kabla ya Rais Magufuli kuchukua hatua hiyo, mwanamke huyo alikwenda mbele ya jukwaa alimoketi Rais, huku akilia kuwa ananyanyaswa na viongozi wa Chadema na kuwa wanataka kumbomolea nyumba yake, bila kufafanua ni kwa vipi.

“Mpe simu yako Mkuu wa Mkoa, halafu atakutafuta na wala usijali, nitamtuma Mkuu wa Mkoa  na haki yako itatendeka, nitalifanyia kazi suala lako,” amesema Rais.

Advertisement
==

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Mpekuzi Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )