Wednesday, July 26, 2017

Mwanamke Mmoja Auawa Kibaha....Polisi Watangaza Vita

Baada ya mkazi wa Mharani kwa Matiasi wilayani Kibaha kukutwa amefariki dunia kwa kuuawa na watu wasiojulikana jana majira ya saa moja usiku, Kamanda wa Polisi mkoani Pwani Jonathan Shana ametangaza mapambano makali ya kuwatia nguvuni wahalifu.

Kamanda Shana amesema kuwa  mwili wa mwanamke huyo aliyetambuliwa kwa jina la Mariamu Omari (31) ulikutwa nje ya nyumba anayoishi mbele kidogo umbali wa mita 40 akiwa anavuja damu nyingi sehemu za usoni na jereha kichwani upande wa kushoto huku muuaji akiwa bado hajafahamika.


"Kufuatia tukio hili jeshi la polisi mkoani Pwani linafanya uchunguzi wa kina kuhakikisha wanaweza kuwabaini waliojihusisha na tukio hilo, Pia wananchi wanatakiwa watoe ushirikiano kwa kuwafichua wahalifu ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

Pamoja na hayo Kamanda Shana amewatahadharisha watu wote wanaojishughulisha na vitendo vya uhalifu kuacha mara moja  kwani jeshi limejipanga kuwasaka na kuwafikisha katika vyombo vya sheria
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )