Thursday, July 6, 2017

Mwanamuziki mkongwe wa Msondo Ngoma Shaaban Dede amefariki

Mwanamuziki mkongwe kutoka Msondo Ngoma Music Band, Shaaban Dede amefariki dunia leo saa mbili asubuhi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa matibabu.

Taarifa hizo zimethibitishwa na mtoto wake wa kiume aliyetambulika kwa jina la Hamad Dede na kusema mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu Mbagala jijini Dar es salaam, na kwamba ratiba na taratibu zote zitatangazwa mara zitapokamilika kupangwa.

Marehemu Dede atakumbukwa kama mmoja wa wanamuziki nguli kutokea nchini Tanzania kwa uwezo wa kucheza na sauti yake pamoja na kuwa mtunzi mahili wa nyimbo mbalimbali  enzi za uhai wake alipokuwa anaimbia bendi tofauti tofauti ni Jazz, Bima Lee, Tabora Mlimani Park na Msondo Ngoma ambako alikuwa anatumikia hadi mauti yanamkuta.
Advertisement
tang
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )