Sunday, July 9, 2017

SORRY MADAM -Sehemu ya 76 & 77 (Destination of my enemies)

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA
Wakiwa katika hali bado ya kushangaa, madam Merya akaona gari mbili za polisi zikisimama katika maegesho yaliyopo mbele yao. Wakashuka watu sita kwenye gari mbili hizo. Kwa haraka madam Mery akamkumbatia Eddy na kumgeuza upande mwengine na kuanza kumnyonya denda huku viganja vyake vyote viwili vikiufunika uso wa Eddy na kuzidi kumnyonya denda Eddy pasipio kumuhofia mtu wa aina yoyote. Shamsa akalishuhudia tukio hilo na kumuonyesha Phidaya kitua anacho kifanya Madam Mery, jambo lililo ipandisha hasira ya Phidaya mara dufu na kuanza kuwafwata madama Merry na Eddy sehemu walipo simama.

ENDELEA
“Eddy hakikisha uwageukii wale askari”
Madam Mery alizungumza kwa haraka kabla hata Phidaya ajawafikia. Kitendo cha Phidaya kufika tu madam Mery akamuachia Eddy na kuingia kwenye gari kuepusha mafarakano yasiyo ya lazima. Phidaya akataka kuingia kwenye gari ili kumchomoa madam Mery ila Eddy akamuwahi na kumkumbatia na kuanza kumnyonya mdomo, huku kwa pembe ya jicho akiwatazama askari hao wanao elekea ndani ya lango la hospitali.

“Niachie”
Phidaya alizungumza huku akijitoa mikononi m wa Eddy. Rahab, raisi Praygod na Sa Yoo walibaki wakiwa na mshangao wasijue ni kitu gani ambacho kinaendela kati ya watu hawa watatu.
“Tuondokeni, Phidaya ingia kwenye gari”
Eddy alizungumza kwa sauti nzito iliyo onyesha msisitizo, taratibu Phidaya akajikuta akiingia kwenye gari hiyo.
“Itabidi kupakatana hapa, siti hazitoshi”
Rahab alizungumza huku akifungua mlango wa mbele, raisi Praygod naye akaingia siti ya mbele, ikabidi  Eddy akae katikati ya madam Mery na Phidaya, huku Shamsa akipakwa na Phidaya na Sa Yoo akipakatwa na madam Mery. Wakaondoka eneo hilo la hospitalini pasipo askari walio kuja kuwatafuta kuwaona.
                                                                                                             ***
   Yassin na vijana wake wakaonye vitambulisho kwa askari walio eneo hilo. Kutoka vitambulisho havina utofauti kabisa na vitambulisho na askari halali, hapakuwa na mtu aliye weza kuwatilia mashaka hata kidogo.
“Tunahitaji kuzungumza na daktari wa zamu”
Yassin alimuambia mmoja wa nesi, aliye kaa sehemu ya mapokezi

“Ngoja niwasiliane naye”
Nesi huyo akanyanyua mkonga wa simu na kumpigia daktari wa zamu na kumuomba aweze kufika sehemu ya mapokezi kuja kuafanya mahojiano na askakari hao. Hazikupita dakika tano daktari wa zamu akafika eneo hilo la mapokezi, akasilimiana na Yassin ambaye hadi sasa hivi hakuna mtu hata mmoja ambaye ameweza kumgundua kwamba yeye ndio gaidi aliye fanya uvamizi masaa kadhaa nyuma.
“Kuna mtu tunahitaji kumuhoji maswali mawali matatu na amelazwa hospitalini hapa”

“Ingekuwa ni vizuri kama ukanieleze jina la mtu huyo anaitwa nani ili tuweze kutazama kwenye vitabu vyetu vya kumbukumbu”
Yassin akatoa simu yake mfukoni na kumuonyesha daktari huyo picha ya Eddy, aliyo itazama kwa muda mchachwe na kuweza kumkumbuka mtu aliye weza kumpatia huduma ya kwanza aliye sadikika kwamba alivamiwa na gaidi.
“Huyu yupo wodini, nilimuhudumia baada ya tukio la uvamizi kutoa”
“Tunakuomba utupeleke kwenye chumba chake”
“Ila kuna usalama kweli?”
“Usalama upo, dokta mbona una wasiwasi”
“Ahaaa haaa hamna”

Daktari alijing’ata ng’ata huku akijaribu kuvuta kumbukumbu ya sura ya Yassin, aliye anza kumtilia mashaka ila kofia aliyo ivaa Yassin kidogo iliweza kumpa matumaini daktari huyo na kujiamini kwamba labda mtu huyo atakuwa sio yeye. Wakafika kwenye wodi ambayo Eddy alilazwa, kila mtu alibaki akishangaa hata daktari mwenyewe.
“Amekwenda wapi huyu mtu?”
Daktari alijiuliza huku akipiga hatua kueleka chooni, akafungua mlango na kukuta hakuna mtu yoyote
“Bosi kwani amevaaje vaaje mtu huyo?”
Khalid alimuuliza Yassin huku akimtazama machoni. Yassin akavuta picha ya jinsi Eddy alivyo valiaa.
“Amevaa shati jeusi, lina mistari mistari myeusi kwenye mikono”

“Shiti bosi, mbona kama huyo mtu nilimuona kwenye maegesho ya magari muda ule tulivyo fika, ila alitupa mgongo na alikuwa akipigana kisi na mkewe sijui”
“Nini?”
“Ndio bosi ninauhakika, kama ni mtu aliye valia shati yeusi basi ninauhakika ndio huyo niliye muona”
“Asante dokta”
Yassin kwa haraka akatoka nje akiwa na vijana wake, wakaingia kwenye magari, wakaondoka eneo la hospitali. Walipo fika getini Yassin akamuamuru kijana wake asimamishe gari ili kumuuliza mlinzi wa getini. Akamuelezea jinsi muonekanano wa Eddy na akamuonyesha picha mlinzi huyo.

“Sijamuona kabisa”
“Je kuna gari lolote lililo toka eneo hili dakika chache?”
“Magari yaliyo toka yapo kama kumi na kila moja limeelekea upande tofauti wa barabara”
“Asante. Ednesha gari”
Yassin alizungumza huku akifunga kioo cha gari na kuondoka eneo la hospitali matumaini ya kumpata Eddy yakiwa yamemuishia kabisa. Hakujua afanye nini ili kumpata kwa maana jiji la Cairo ni kubwa sana na ni ngumu kumtafuta mtu mmoja tu.
                                                                                                      ***
   Breki ya kwanza ikawa nyumbani kwa raisi Praygod. Wakashuka kwenye gari kila mmoja akiwa amechoka sana huku matumbo yao yakisumbuliwa na njaa waliyo dumu nayo kwa muda mrefu sana. Sa Yoo moja kwa moja akaelee lilipo friji akafungua na kutoa chupa ya soda na kuanza kuigugumia, bila ya mapumziko.
“Mmmm best utapaliwa”
Shamsa alizungumza huku akitabasamu
“Mmmm bora kupaliwa kuliko hii kiu niliyo kuwa nayo. Yaani tangu asubuhi nilivyo ondoka hotelini sijakula chochote hadi muda huu”

“Ehee hivi ilikuwaje kuwaje hadi mukaja hospitalini?”
“Tulikuja kukuangalia, tulisikia kwamba uliwahishwa hospitalini na madam Mery baada ya wewe kuwa katika hali mbaya.”
“Tulivyo ondoka asubuhi nilikuacha ulale kwa maana uliletwa umelewa chapachapa. Sasa muda tunarudi hotelini tukaambia kwamba umewahishwa hospitalini, kufika madam Mery anatuambia kwamba umefariki. Sasa muda ule ninakuona pale mapokezi, niliingiwa na woga kiasi kwamba nikataka kuondoka. Ila nilijikaza na kukufwata”
“Hapo sasa nimeanza kupata picha?”
“Picha gani?”

“Unajua  jana usiku kichwa kiliniuma sana, nikajisahau kama nimekunywa pombe. Nilichukua zile dawa zako za kukuzuia maumivu ya kichwa, nikazinywa. Kuanzia hapo sikuelewa nini kinacho endelea. Kuja kustuka najikuta nipo mochwari”
“Mochwari…….??”
“Yaani wee acha tu, kunatisha kama nini na kuna ubaridi mkali”
“Jamani mabinti tusaidiane kupika”
Rahab alizungumza na kuyakatisha mongezi ya Sa Yoo na Shamsa, hapakuwa na aliye bisha, wakaingia jikoni na kuanza kusaidiana kupika.
“Mudabidi muweke tofauti zenu pembeni sasa”
Raisi Praygod alizungumza huku akiwa anawatazama Eddy, Phidaya na madam Mery alio kaa nao kwenye sebleni.

“Ila muheshimiwa haiwezekani, huyu malaya kumkisi mume wangu tena wa ndoa”
“Phidaya cha kumtusi mwenzio”
“Ahaaa kwa hiyo unamtetea huyo malaya, si ndio”
“Phidaya hembu kuwa na lugha ya busara. Tambua upo wapi na unazungumza na watu wa aina gani”
Raisi Praygod alizungumza kwa sauti ya ukali kidogo na kumfanya Phidaya kukaa kimya, ila jazba yake bado inautawala moyo wake.

“Muheshimiwa ninaomba nizungumze kitu, ambacho kilinifanya mimi kuweza kufanya nilicho kifanya”
“Zungumza”
“Mimi nilikuwa ni miongoni mwa wanachama wa D.F.E. Niliingia kwenye chama hicho kutokana nilikuwa na musiano ya kimapenzi na Mzee Godwin ambaye kwa sasa ni raisi wa Tanzania.”
Madam Mery alizungumza kwa sauti ya upole iliyo jaa unyeyekevu.
“Lengo kubwa lilikuwa ni la kumteketeza Eddy ambaye ni mtoto wa mzee Godwin, tena wa kumzaa naamini unalitambua hilo muheshiwa, kwamba Eddy huyo hapo ni mtoto wa Godwin”

Raisi Praygod akatingisha kichwa akiashiria kwamba anatambua swala hilo.
“Ukiachilia mbali swala zima la kumuua Eddy, ila D.F.E, inajishuhulisha na mambo mengi duniani. Ni mtandoa mmoja wa siri ambao ni mkubwa na wenye nguvu kulia hata kundi la Alquida. D.F.E inamatawi karibia dunia nzima. Na ndio iliyo pelekea wewe kuangushwa kwenye uchaguzi kwa maana ndani ya serikali yako kulikuwa na watu wa ngazi ya juu ambao walikuwa wakiungana na Mzee Godwin.”

“Tukiachana na hayo tuje kwenye wale askari tulio waona pale hospitalini. Naweza kuwaambia kwamba hakuna askari pale. Yule jamaa mrefu anaitwa Yassin alikuwa ni bodigadi wangu kipindi nipo kwenye mtandao wa D.F.E, ndio maana niliweza kumtambua haraka sana nilipo weza kumuona pale kwenye maegesho. Ninaimani walikuja kwa lengo la kumteka Eddy. Laiti wangemuona sisi wote tungeangamia, kwa maana Yassin huwa ni mtu asiye na huruma kwa mtu ambaye amekusudia kumuua"

Phidaya akajikuta akishusha pumzi, kwa maana anamtambua vizuri mzee Godwin na ndio mtu aliye sababisha yeye kuingia katika matatizo ya kupotezana na mume wake.
“Tupo katika hali ya hatari, tunatakiwa kuwa tayari kwa lolote muda wowote kuanzia sasa.”

“Sasa tutafanyaje jamani?”
Raisi Praygod alizungumza kwa unyonge akionyesha hivi hivi ni dhaifu katika swala hilo.
“Muheshimiwa naomba hiyo kazi uniachie mimi, ninaimani kwamba  kila jambo litakwenda sawa. Nitahakikisha kwamba ninamuu mzee Godwin”
“Honey sio kiurahisi kama unavyo hisi. Wewe mwenyewe unamjua baba yako alivyo na roho mbaya”
“Hakuna mtu mwengine anaye weza kupambana na mzee Godwin zaidi yangu. Inabidi tufanye mpango wa kurudi Tanzania”

“Eheeee Tanzania!!?”
“Ndio honye ni lazima turudi Tanzania, kule ndio kwetu. Nilazima kuitetea nchi yangu kwa maana kwa sasa wananchi wanapitia kwenye kipindi kigumu sana”
“Baby mimi sirudi nitakaa hapa hapa?”
Phidaya alizungumza kwa woga mkubwa sana. Sa Yoo akaingia sebleni na kuwatazama watu wote kwa haraka akagundua kuna jambo ambalo linaendelea eneo hilo
“Jamani munaombwa muje mezani chakula kimesha ivaa”
“Sawa tunakuja”
Raisi Praygod alijibu, Sa Yoo akaondoka na kuacha ukimya ukitawala. Hapakuwa na mtu aliye zungumza jambo lolote. Madam Mery akanyanyuka na kueleka kwenye meza na kuwaacha Phidaya, Eddy na raisi Praygod.

“Jamani natangulia mezani”
Raisi Praygod aakanyanyuka na kuondoka. Eddy akamtazama Phidaya usoni
“Mke wangu tunabidi kurudi Tanzania. Nahitaji kukulinda siwezi kukuacha ukae mbali nami?”
“Ila honey naogopa”
“Usiogope nitakulinda hadi mwisho wa maisha yangu”
Eddy alizungumza huku taratibu akimvuta Phidaya kifuani mwake na kumkumbatia.

Advertisement
tang
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )