Monday, July 17, 2017

SORRY MADAM -Sehemu ya 78 & 79 (Destination of my enemies)

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA

Macho ya Eddy yakaweza kuona msafara mzima wa raisi Praygod unavyo ingia katika sehemu ya abiria wanao safari. Macho ya Eddy yakagongana na macho ya Manka ambaye anamtambua vizuri, akaona jinsi Manka anavyo mshangaa kiasi cha kuhisi amegundulika. Kitendo cha raisi Praygod kusimama na kuzungumza na Manka, kikaanza kupandisha hasira ya Eddy, akataka kuruka katika vizuizi vilivyopo katika upande wake na kuelekea upande wa mzee Godwin anaye lindwa na askari wengi, ila kwa haraka raisi Praygod aliye valia kofia kubwa la kizee akamuwahi na kumshika mkono kwa nyuma Eddy.
“Hapa sio eneo lake Eddy utasababisha mpango kuharibika”

ENDELEA
“Ok nimekuelewa muheshimiwa”
Eddy alizungumza huku akishusha pumzi ila macho yake, akimtazama jinsi mzee Godwin anavyo zidi kutokomea mbele ya macho yake. Wote kwa pamoja wakakutana sehemu ya maegesho ya magari.

“Tumefika salama, tunamshukuru Mungu”
Raisi Praygod alizungumza huku akiwatazama watu wote. Madereva taksi kama kawaida yao, hawakusita kuweza kuchangamkia tenda ya kuwachukua wageni hao.
“Taksi mbili zinatosha”
Madam Mery alizungumza huku akiwatazama madereva wengine ambao, waliwahiwa na madereva wawili walio wahi kufika eneo walilo simama.
“Inabidi tujue tunaeelekea wapi kwa sasa?”
“Tupeleke bahari beach naamini itakuwa ni sehemu sahihi kwa sisi”

“Sawa munaweza kuingia kwenye gari”
Eddy akaingia gari moja akiwa na Phidaya, Sa Yoo na Shamsa. Huku raisi Praygod akiingia gari moja akiwa na Rahab pamoja na Madam Mery. Safari ikaanza huku kila mmoja akiwa kimya ndani ya gari akitafakari lake.
‘Raisi Godwin anawatakia watanzania mapumziko mema ya sikukuu’
Sauti ya redio ya gari walilo  panda Eddy, ilisikika vizuri kutoka kwenye moja ya kituo cha redio jambo lililo mfanya dereva taksi kuguna.
“Mbona unaguna ndugu?”
Eddy aliuliza huku akimtazama dereva huyo.
“Kusema la ukweli, tulikosea sana kumchagua raisi huyo. Nchi ameivuruga vuruga na sasa”

“Ameivuruga kivipi?”
“Yaani kwa sasa, anataka kubadilisha hadi mfumo wa utawala. Anataka kutuletea maswala ya mfalme Mswati hapa”
“Duuu!!”
“Ndio yaani anataka kuweka utawala wa ufalme na atashikilia madaraka hadi anakufa na akifa anamrithisha mwane, sasa huo si ujinga kweli”
“Poleni sana”
“AAhaa tumesha poa, ila kusema la ukweli nchi kwa sasa haina uhuru kabisa. Wanao nufaika ni watu wachache sana sisi huku chini tunazidi kuumia. Natamani hata raisi Praygod angeendelea kushikilia nchi”
“Ilikuwaje hamkumchagua kwenye uchaguzi?”
“Ahahaa si unajua ujinga wa kushikiwa masikio. Watu walidai wanataka mabadiliko ya chama cha upinzani sasa mabadiliko ndio haya.”

Dereva huyo alizungumza huku machozi kwa mbali yakimlenga lenga. Ni mmoja wa watanzania ambao wanajutia kabisa kufanya chagua mbalo walihisi ni sahihi kwa nchi yao ila si sahihi kama wanavyo jionea sasa. Wakafika katika hoteli ya bahari beach. Madam Mery akawalipa madereva taksi hao kisha wakaingia ndani na kupokelewa na wahudumu. Wakakodi vyumba vine kwa ajili ya mapumziko.
“Jamaninahitaji kuelekea ilipokuwa nyumba yangu”
Eddy alizungumza wakiwa katika meza moja ya chakula wakijipatia chakula cha mchana.
“Honey unahisi nyumba yetu inaweza kuwepo hadi leo?”
“Nahisi ipo na kama itakuwa haipo basi hakuna kitu cha kufanya.”

“Basi naomba twende wote”
Shamsa alizungumza huku akimtazama Eddy usoni, akisubiria jibu ambalo Eddy atazungumza.
“Itakuwa ni vizuri, Shamsa unaweza kuweka ulinzi kwa baba yako”
Phidaya aliwahi kujibu hata kabla Eddy hajatoa jibu, kutokana ni mbele za watu Eddy hakujibu kitu chochote zaidi ya kukaa kimya.
“Basi nitawapatia pesa kidogo muweze kwenda”
Madam Mery alizungumza na hapakuwa na aliye weza kukataa kwa maana Eddy hakua na kiasi chochote cha pesa. Walipo maliza kupata chakuka cha mchana, madam Mery akampatia Eddy laki moja, kati ya pesa alizo zitoa kupitia ATM, mara baada ya kufika uwanja wa ndege.

“Shukrani”
Eddy na Shamsa wakatoka nje ya hotel, wakakodi taski na kuelekea ilipo kuwa nyumba yake. Hawakuchukua muda mrefu kutokana na foleni kuwa ndogo.
“Dereva simamisha hapo kwenye hilo geti jeusi”
Dereva akatii kama alivyo elekezwa na mteja wake. Akasimamisha mbele ya geti la nyumba ya Eddy, ambaye hakushuka kwanza kuangalia mazingira ya eneo hilo. Utulivu wa eneo hilo, ukampa matumaini ya kushuka kwenye gari.
“Unaweza ukatusubiria hapa nje?”
“Hakuna shaka mkuu”
“Shika kwanza hii ya nauli tuliyo jia, tukichelewa unaweza ukaenda”

“Hakuna tabu kiongozi”
Shamsa akashuka kwenye gari, wakapiga hatua chache hadi kwenye geti. Vumbi jingi lililopo kwenyegeti kidogo likawapa maswali ambayo hawakuwa na majibu nayo kwa haraka haraka. Eddy akataka kugonga mlango ila Shamsa akamshika mkono.
“Ngoja kwanza”
Shamsa akasukuma kigeti kidogo cha kuingilia kwa bahati nzuri akakuta hakijafungwa kwa ndani. Taratibu Shamsa akaanza kuingia kwa tahadhari kubwa, wingi wa majani na yaliyo marefu kwenda juu, yaliashiria fika kwamba nyumba hiyo haina uangalizi wa mtu yoyote.
“Ingia”
Eddy akaingia na kushuhudia hali ya uchakavu iliyopo katika nyumba yake. Wakazidi kutembea kueleka mbele na kufika katika lango la kuingilia ndani kabisa. Mlango huo ulijaa matobo mengi, ambayo Eddy anakumbuka yalitokana na mashambulizi ya wanajeshi kipindi cha nyuma.

“Hawaishi watu”
Shamsa alizungumza huku akitangulia kuingia ndani na kumuacha Eddy akiwa amesimama akiendelea kutazama jinsi nyumba yake hiyo ilivyo chakaa. Wakaendelea kuchunguza maeneo yote ya nyumba yake hadi kwenye chumba chake cha siri, alicho kichimbia chini ya arthi.
“Hiki chumba sijawahi kukiingia”
“Hiki ni chumba changu cha siri ambacho si rahisi kwa mtu kuweza kukigundua, japo nakumbuka askari walijaribu kukivamia ila hawakuweza”

“Nimeimisi sana hii nyumba, ila Eddy unaonaje takaja kuishi tena hapa”
“Itakuwa hakuna usalama, endapo kukigundulia kuna watu wanaishia. Kumbuka mpango wetu”
Eddy akasimama kwenye moja ya ukuta, akatoa moja ya picha kubwa iliyopo ukutani hapo. Sehemu ilipokuwa picha hiyo kuna batani zilizo jificha ambazo zinaendana kabisa na rangi ya ukuta. Eddy akaminya namba hizo na kuingiza namba ya siri. Sehemu ya ukuta hiyo iliyo chongwa usawa wa ukuta ikafunguka, hadi Shamsa akabaki ametoa macho.
“Nifwate”

Eddy alizungumza huku akiingia ndani ya chumba hicho. Akaminya moja ya swichi iliyopo kwenye mlango wa chumba hicho. Mwanga mkali ukatawala ndani ya chumba hicho, na kumfanya Shamsa kuzidi kushangaa. Vibunda vingi vya dola za kimarekani, vimepangwa nusu ya chumba hicho, kiasi kwamba viliwapita hawa wao urefu. Upande mwengine wa chumba hicho kumejaa silaha nyingi za kila aina.
“Eddy……….!!! U…uu…mezitoa wapi hizi pesa?”
Shamsa aliuliza huku akiwa amezisogelea pesa hizo, akaanza kushika kibunda kimoja baada ya kingine akionekana kuto wahi kuona kiashi kikubwa cha pesa kama hicho.
“Hizi pesa nilizitoa kwenye akaunti zangu zote mara baada ya kukabidhiwa uwaziri wa wa ulinzi, baadhi ya pesa nilizipata kule Somalia kipindi kile nilipo kuwa ninaitafuta familia yangu”

“Ahaaa ni zile pesa tulizo zipeleka kwenye bank ya Bacrayce, na ndipo mara ya kwanza kumuona madama Mery”
“Swadataaa hujakosea. Nilichanganya na pesa nyingine nyingine na zote nikaziingiza humu, sikuwaambia kwa maana niliona si vizuri”
“Kweli wewe ni msiri, ina maana hata Phidaya mwenyewe hafahamu?”
“Hafahamu, mtu aliye kuwa anafahamu ni marehemu mwanangu Junio”
“Junio…..?”
“Ndio, tena twende tukaangalie makaburi yao”
Eddy akachukua vibunda vitatu vya pesa, kimoja akampatia Shamsa na viwili akaviweka kwenye suruali yake. Akachukua bastola moja na magazine mbili, kisha wakatoka katika chumba hicho na kukifungu.
“Usimueleze mtu yoyote juu ya hichi chumba”
“Sawa, niamini”

Wakatoka na kuzunguka nyuma ya nyumba hiyo palipo na makaburi ya Junio, mama Eddy na kaburi la Phidya.
“Sasa Eddy, kaburi la mama, si litakuwa halina mtu, kwa maana yeye mwenye si yupo hai?”
“Eheee nimekumbuka, nahitaji kulivunja na kuona ndani kama kweli aliye zikwa alikuwa mke wangu au laa”
“Tulivunje sasa hivi?”
“Ndio, jambo linalo wezekana leo lisingoje kesho”
Wakarudi ndani hadi stoo, ambapo wakavaa manguo ya kufanyia kazi pamoja na kofia ngumu kama wanazo vaa wakandarasi wa barabara. Wakachukua nyundo mbili kubwa wakatoka nje hadi yalipo makaburi.
“Vunja huko na mimi nivunje upande huu”
“Unaonaje Eddy, tukavunja eneo la huku kwenye msalamba”
“Sawa”

Kazi ikaanza kuvunja kaburi hilo lililo tengenezwa na saruju imara. Haikuwa kazi rahisi kwao, ila hawakukata tama, hadi wakafanikiwa kuweza kuweza kufungua mfuniko mzito wa kaburi hilo. Kila mmoja akabaki akiwa ameduwaa. Kwa maana hawakukuta jenza ambalo Phidaya alizikiwa.
”Limekwenda wapi?”
Shamsa aliuliza huku akidumbukia ndani ya kaburi hilo. Taratibu Shamsa akachuchumaa, na kuangalia sehemu ya mbele yake, ambapo kulichomekwa msalaba. Akakuta kuna uwazi mdogo.
“Vipi mbona umechuchumaa”
“Hapa kuna uwazi”
“Uwazi?”
“Ndio”
Ikabidi na Eddy naye adumbukie kwenye kaburi hilo, uwazi huo mdogo, ukamfanya Eddy kuingiza mkono pasipo kuhofia kitu chochote. Akagundua kuna kiji mlango.

“Hembu lete nyundo”
Kwa harka Shamsa akatoka nje ya kaburi na kumpatia nyundo moja Eddy, kisha na yeye akarudi ndani ya kaburi.
“Hembu sogea pembeni kidogo”
Shamsa akafanya kama alivyo elekezwa, Eddy akaanza kuvunja uwazi  huo, hapo ndipo wakakutana na mlango huoo wa mbao wenye ukubwa mbao unatosha kabisa kwa jeneza kupita. Eddy akauvunja mlango huoo, giza lililopo ndnai ya sehemu hiyo kulipo mlango huo, ukawafanya washindwe kuweza kuona ni kitu gani kilichopo ndani.
“Unataka kuingia humo ndani?”
Shamsa alimuuliza Eddy huku akiwa amemtolea macho.
“Hapana nahitaji tochi”
“Tochi nimeiona kule stoo”
“Kailete”
Shamsa akatoka na kuelekea hadi stoo, akachukua tochi moja kubwa, na kurudi hadi sehemu ya kaburi, ila kitu kilicho mshangaza hakumuona Eddy katika eneo hilo. Kwa haraka huku wasiwasi ukiwa umejaa, akaingia ndani ya kaburi.


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )