Saturday, July 29, 2017

Trump Amtumbua Mkuu wa Utumishi Serikalini

Rais Donald Trump wa Marekani amemteua Waziri wa Mambo ya Ndani, John Kelly kuwa mkuu wa utumishi wa Serikali baada ya kumwachisha kazi Reince Priebus.

Priebus amefanya kazi kwenye Serikali hiyo kwa muda wa miezi sita tu.

Baada ya miezi kadhaa ya uvumi kuhusu hatima ya Priebus, Trump ametangaza uamuzi wake kwenye mtandao wa Twitter akiwasili mjini Washington.

Awali, Trump alitoa hotuba jijini New York ambayo aliitumia kummwagia sifa Kelly kwa kazi anayofanya katika wizara hiyo.

Amesema ,"Nina furaha kuwafahamisha nimemteua waziri John Kelly kuwa mkuu wa utumishi wa Serikali katika Ikulu."

Advertisement
==

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Mpekuzi Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )