Monday, July 3, 2017

Yaliyojiri Bungeni Katika Kikao Cha 58 Cha Mkutano Wa Saba Wa Bunge La 11 Leo Tarehe 03 Julai, 2017

*YALIYOJIRI BUNGENI KATIKA KIKAO CHA 58 CHA MKUTANO WA SABA WA BUNGE LA 11 LEO TAREHE 03 JULAI, 2017*.

1.Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ndiyo yenye jukumu kuu kisheria la kukusanya mapato ya Serikali.

2.TRA ilianza rasmi kukusanya kodi ya majengo kwa Halmashauri 30 kati ya 183 kuanzia Octoba 2016.

3.Katika kipindi cha Julai-Septemba, 2016,Halmashauri 30 ziliweza kukusanya shilingi milioni 3,399 sawa na asilimia 24 ya lengo la kukusanya milioni 14,502.

4.Kati ya Octoba 2016 hadi Aprili 2017, jumla ya Shilingi Milioni 10,652.6 zilikusanywa sawa na aslimia 22.0 ya lengo la kukusanya Shilingi Milioni 48,340.2.

5.Ufanisi huu ni sawa na wastani wa makusanyo ya Shilingi Milioni 1,521.8 kwa mwezi.

6.TRA imekusanya kodi ya majengo kwa ufanisi zaidi ikilinganishwa na Halmashauri.

7.Serikali imeaainisha maeneo yote nchini yanayofaa kwa Kilimo cha umwagiliaji na kuandaa Mpango Kabambe wa kuendeleza Kilimo cha umwagiliaji.

8.Mpango huu utahusisha matumizi ya maji ya maziwa makuu ikiwemo Ziwa Victoria kwa ajili ya umwagiliaji wa kutumia teknolojia zinazotumia maji kwa ufanisi.

9.Awamu ya tatu ya Mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini (REA) umeanza kwa Nchi nzima tangu Mwezi Machi, 2017.

10.Serikali imeweka utaratibu ambapo posho za viongozi wa Serikali za Vijiji na Vitongoji zinalipwa na Halmashauri kupitia asilimia 20 inayotengwa kutokana na mapato ya ndani ya Halmashauri na kurejeshwa kwenye Vijiji.

11.Serikali inakusudia kuliweka kwenye Sheria ya Fedha suala la kutenga asilimia 20 kama posho za viongozi wa Serikali.

12.Serikali imetenga Shilingi Milioni *557.3* kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba pamoja na ujenzi wa vituo vya Afya na Zahanati.

13.Katika mwaka 2015/16 jumla ya meta za ujazo wa miti zipatazo *767,946.46* zilivunwa kutoka kwenye mashamba ya Serikali na kuingizia Serikali jumla ya Shilingi *58,312,894,416.20*

14.Mapato yanayotokana na zao la mbao,ni wastani wa Shilingi *Bilioni 18.3* kwa mwaka.

*Imeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO*
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )