Tuesday, August 22, 2017

Breaking News: Tundu Lissu Akamatwa na Jeshi la Polisi Akiwa Kisutu

Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu amekamatwa  leo Jumatatu mchana akitokea Mahakama ya Kisutu.

Mwanasheria huyo alikuwa na kesi ya tuhuma za uchochezi lakini pia alikuwa ni wakili kwenye kesi inayomkabili mfanyabiashara Yericko Nyerere mahakamani hapo.

Akielezea ilivyokuwa Ofisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene amesema wakati gari la Lissu likiwa liko getini tayari kwa kutoka, likazuiwa na nyuma ya gari yake pia likasimama gari jingine likiwa na askari polisi wenye silaha, kisha wengine wakamfuata na kumwambia yuko chini ya ulinzi na atakiwa kwenda Central Police.

Baada ya hapo, wakamtaka ashuke kwenye gari lake na apande gari jingine la kwao kwa ajili ya kuelekea Central Polisi.

Tundu Lissu amekamatwa leo tarehe 22 Agosti 2017 zikiwa zimepita siku tatu toka alipotoa taarifa ya ndege ya Tanzania  'Bombadier Dash Q400' kuzuiliwa nchini Canada kutokana na amri ya mahakama

==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )