Wednesday, August 30, 2017

Halima Mdee alia na polisi, asema kuna matapeli wanamsumbua

Mbunge wa Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Halima Mdee amesema kuwa anasikitishwa na jeshi la polisi kushindwa kuwakamata matapeli ambao wamekuwa wakitapeli wananchi kwenye mitandao kupitia jina lake.

Amesema kuwa ni muda mrefu alishatoa taarifa  jeshi la polisi kuhusu watu hao wanaotumia jina lake kwenye mitandao ya kijamii na kujifanya kutoa mikopo yenye riba ndogo na kuwatapeli wananchi pesa zao.

“Wanaojitambulisha kutoa mkopo kwa jina langu ni matapeli, sihusiki na chochote na hao matapeli na nmeshatoa taarifa polisi inaonekana hawakamatiki” amesema Halima Mdee

Advertisement
==

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Mpekuzi Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )