Wednesday, August 16, 2017

Majeruhi watatu ajali ya Wanafunzi Arusha Kurejea Nchini Kesho Kutwa

Watoto watatu walionusurika kwenye ajali ya basi la wanafunzi wa Shule ya Lucky Vincent ambayo ilipoteza maisha ya wanafunzi 32, wanatarajia kurejea nchini August 18, 2017 baada ya kupatiwa matibabu Marekani.

Mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu ambaye alikuwa mstari wa mbele kusimamia shughuli ya kuwasafirisha, amesema ratiba ya mapokezi itaanza mapema zaidi ambapo itakuwa saa Moja asubuhi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro, ‘KIA’ ambapo Makamu wa Rais Samia Sulu Hassan atawaongoza Watanzania.

”Watawasili tarehe 18, 2017 wiki hii wakiwa wanaletwa na ndege ile ile iliyowachukua na ratiba inaanza mapema kidogo saa moja asubuhi, wananchi na wanafamilia wanatarajiwa wawe wamefika uwanja wa KIA, Kutakuwa na viongozi mbalimbali na tunatarajia makamu wa Rais kuwa mgeni rasmi.”  Amesema  Lazaro Nyalandu.
==


Advertisement
Punguzo la Bei 20% msimu huu wa Idd.Agiza saa hii ya Automatic, na lipa mzigo ukifika majiji yote TanzaniaAdvertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )