Monday, August 14, 2017

MCT Yatangaza Ripoti ya Uchunguzi wa Uvamizi wa Studio za Clouds TV

Baraza  la Habari Tanzania (MCT) limezindua Ripoti ya Hali ya Vyombo vya Habari hapa nchini kwa mwaka 2016 (State of the Media Report) ambapo ripoti hiyo hutolewa kila mwaka ili kuushirikisha umma

Pia Baraza hilo linatoa ripoti kuhusu kuvamiwa kwa Studio za Clouds Media na kubaini jinsi tukio hilo lilivyoathiri uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa uhariri.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Katibu wa Baraza hilo amesema ripoti hiyo haina lengo baya, bali ni kuweka bayana hali ya tasnia ya habari na kwamba hambo hilo si mara ya kwanza kwani baraza hilo limekuwa likitoa ripoti kama hizo kila mwaka.

“Hatujafanya uchunguzi huu kwa kuwa tuna mapenzi na Clouds Media wala kwa sababu tuna mahusiano na Mkuu wa Mkoa, badala yake tumetoa ripoti hii kwa mujibu wa katiba ya MCT,” alisema katibu.

==>Tazama hapo chini

Advertisement
==

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Mpekuzi Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )