Tuesday, August 15, 2017

Mrema Amshukuru Rais Magufuli kwa Kumsaidia Kupona Kansa

Mwenyekiti wa Bodi ya Msamaha kwa Wafungwa (Parole), Augustine Mrema ametoa shukrani zake kwa Rais John Magufuli kwa kumsaidia kupata matibabu nchini India na kufanikiwa kupona ugonjwa wa kansa.

Mrema alisema kwa sasa utendaji wake wa kazi utaimarika kwa kuwa ameshapona ugonjwa uliokuwa ukimsumbua na kushindwa kutumikia wananchi na Taifa.

Akizungumza mbele ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mama Mwokozi jijini Dar es Salaam, alisema kuanzia sasa atamsaidia vizuri Rais katika nafasi yake ya kuwatetea wafungwa kupitia msamaha wa Bodi ya Parole.

Alisema amefikia hatua ya kutoa shukrani kwa sababu ya muujiza aliopata kutoka kwa viongozi wa Serikali na dini waliomuombea.

Paroko Kiongozi wa kanisa hilo, Cathbert Magaga aliwataka waumini wengine kuiga mfano wa Mrema wa kutoa shukrani na siyo kunyamaza kwa kuwa Mungu atawasaidia.

Advertisement
==

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Mpekuzi Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )