Saturday, August 26, 2017

Ofisi za Mawakili Fatma Karume na Lawrence Marsha Zimeteketea kwa Moto

Ofisi ya IMMMA House inazomilikiwa na wanasheria kadhaa akiwepo Fatma Karume na Lawrence Masha   zimeungua moto usiku wa kiamkia leo ambapo chanzo cha moto huo bado hakijafahamika.

Wakili Fatma Karume kwa siku za hivi karibuni alisikika sana alipokuwa akimtetea Tundu Lissu mara baada ya kukamatwa uwanja wa ndege alipokuwa akisafiri kwenda Rwanda.

Taarifa za awali ambazo hazijathibitishwa na Jeshi la Polisi kutoka kwa majirani wa eneo hilo wamedai kuwa walisikia mlio mithili ya bomu wakati wa usiku.

Advertisement
==

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Mpekuzi Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )