Thursday, August 17, 2017

Prof. Mkumbo Ammwagia Sifa Raila Odinga.....Adai ni baba wa Demokrasia Afrika

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo amepongeza hatua zilizochukuliwa na kiongozi wa muungano wa vyama vya upinzani nchini Kenya (NASA), Raila Odinga za kwenda mahakamani kudai haki yake.

Amesema kuwa kipindi ambacho kina Odinga wanapambana kupigania mageuzi wakati wa muhula wa pili wa utawala wa Rais Daniel Arap Moi, Uhuru Kenyatta yeye alikuwa kivulini

Prof. Mkumba amesema kuwa Raila Odinga ni mwanasiasa aliyekomaa kidemokrasia hivyo anafaa kuitwa baba wa demokrasia barani Afrika huku akiwataka wanasiasa kuiga mfano huo.

“Ahsante sana Raila Odinga kwa hakika maamuzi uliyofanya kwenda mahakamani kutafuta haki ni maamuzi sahihi, wewe ni baba wa Demokrasia katika ukanda huu,”amesema Prof. Mkumba.

"Huyu Kenyatta ni beneficiary. Wakati akina RAO wakipambana na akina Moi yeye alikuwa kivulini. Tuwe wa kweli" amesisitiza Kitila Mkumbo 

Uchaguzi mkuu nchini Kenya umefanyika hivi karibuni ambapo mgombea kutoka chama tawala cha Jubilee, Uhuru Kenyatta aliibuka mshindi na kumbwaga Raila Odinga 

==>Chek apo chini
 
==


Advertisement
Punguzo la Bei 20% msimu huu wa Idd.Agiza saa hii ya Automatic, na lipa mzigo ukifika majiji yote TanzaniaAdvertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )