Wednesday, August 30, 2017

Rais wa Simba, Evans Aveva Mahakamani Tena Leo

Upande wa Mashtaka katika kesi inayomkabili Rais wa Simba, Evans Aveva na Makamu wake  Geofrey Nyange ‘Kaburu’  leo umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa wamekusanya nyaraka za upelelezi na zimepelekwa kwa mtaalamu wa maandishi.

Hayo yamesemwa na Wakili wa Serikali, Estazia Willson mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa wakati kesi hiyo ilipoitishwa kwa ajili ya kutajwa.

Wakili Wilson amedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, pia wamekusanya nyaraka na zimepelekwa kwa mtaalam wa maandishi, hivyo wanasubiri ripoti.

Hakimu Nongwa ameahirisha kesi hiyo hadi September 8, 2017.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )