Tuesday, August 15, 2017

Shamsha Ampongeza Rais Magufuli kwa Kuinyoosha Nchi

Malikia wa filamu bongo 'Shamsa Ford' amefunguka kwa kumshukuru Rais Magufuli kwa namna anavyoendesha nchi kwa sasa huku akidai ameweza kuwasaidia vijana kuwa wabunifu katika maisha yao tofauti na awali.

Shamsa ameeleza hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram, baada ya kuwepo maneno ya muda mrefu kwa jamii hasa vijana kulalamika maisha yamekuwa magumu kwa kuwa Rais Magufuli amebana baadhi ya mirija ambayo vijana hao walikuwa wanaitumia kupata mahitaji yao ya kuendesha familia zao kila leo.

"Tunalalamika maisha ni magumu sana labda kwa kuwa hatujazoea hii hali, ila mimi nakupongeza sana Rais wangu Magufuli kwa kazi unayoifanya. Kwanza umetusaidia vijana kuwa wabunifu kila siku", ameandika Shamsa.

Pamoja na hayo, Shamsa ameendelea kwa kusema "walikuwa wamezoea kupewa tu pesa na kazi hawafanyi ila kwa sasa anaona kila kijana anafanya kazi kwa bidii na kuheshimu pesa vizuri. Hivyo suala hilo limeweza kusaidia hata kwa uchumi wa nchi kukua kutokana na kwamba kila kijana anafanya kazi kwa bidii".

Kwa upande mwingine, Shamsa amemuombea Rais Magufuli Mungu Amlinde amlinde na mabaya anayoombewa na baadhi ya watu ambao wanatamani yamfikie ili asiweze kutimiza yale aliyokusudia kuyatekeleza kwa wananchi wa Tanzania.
==


Advertisement
Punguzo la Bei 20% msimu huu wa Idd.Agiza saa hii ya Automatic, na lipa mzigo ukifika majiji yote TanzaniaAdvertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )