Tuesday, August 15, 2017

Shilole Apangua Madai Ya Kuiba Mume Wa Mtu

Msanii Zuwena Mohamed 'Shilole' amekanusha zile tetesi zilizokuwa zinamuandama za kuiba mume wa mtu na kudai jambo hilo halina ukweli ila watu wamezoea kumuongelea vibaya kwa kuwa yeye ni mtu maarufu.
 
Shilole amefunguka hayo baada ya kuandamwa takribani majuma mawili hivi sasa kuwa amevunja ndoa ya mwanamke mwenzake na hatimaye kumchukua mwanaume huyo jumla jumla na  kukaa naye nyumbani kwake jambo ambalo lilipelekea watu wengi kumtolea maneno kwenye mitandao ya kijamii.

"Siyo kweli, sijawahi kuiba mume wa mtu mimi. Ila huyo mwanaume ni kweli alikuwa na mke lakini walisha achana siku nyingi hivyo kuwa naye siyo sababu ya kuivunja ndoa yao", alisema Shilole.

Pamoja na hayo, Shilole ameendelea kwa kusema kuwa anatarajia kuolewa siku si nyingi kutokea sasa japo hakutegemea jambo hilo kutokea kwake tena.

"Panapo majaliwa nategemea kuolewa mwezi wa 10 au 11 mwaka huu haupinduki lazima ntakuwa nimeolewa. Kiukweli sikutamani kabisa kuolewa kwa sababu nilishaufunga ule ukurasa lakini imetokana tu ushawishi wa mwanaume niliyekutana naye. Wakwe zangu wamenipokea vizuri siku nilivyotambulishwa na wamenipenda kiukweli kwa kuwa mimi nipo vizuri kila sehemu", alisema Shilole.

Katika hatua nyingine, Shilole amewataka watu watambue kuwa yeye siyo chanzo cha migogoro ya kuvunjika kwa ndoa ya mpenzi wake wa zamani Nuh Mziwanda kama watu wanavyodhani.

"Mimi kiukweli siyo chachu ya ndoa ya Nuh Mziwanda na Nawal kuvunjika hata kidogo kila mmoja ana mambo yake anafanya lakini nashangaa kwanini nahusishwa mimi kwenye mambo yao yakitokea, maana hata wakigombana chumbani wanasema mimi ndiyo chanzo. Siyo sawa kiukweli maana yameshapita ile kitu lakini nashangaa bado kuendelea kuwepo kwenye midomo ya watu", alisisitiza Shilole.

Kwa upande mwingine, Shishi amedai hata akiolewa hatoweza kubadilika kwa kuwa kazi yake haiwezi kuingiliana na ndoa yake hata siku moja
Advertisement
tang
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )