Friday, August 4, 2017

SORRY MADAM -Sehemu ya 80 & 81 (Destination of my enemies)

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA  
Eddy akabaki akiwa ametoa macho, huku akiitazama picha ya John, wasiwasi mwingi ukamjaa, akifahamu kwamba ni lazima John naye anajipanga kwa kuweza kulipiza kisasi dhidi yake. Madam Mery akageuka na kuwatazama wasichana hao, akastuka na kumgeukia Eddy.
“Vipi mbona umestuka”
“Hao wasichana ni hatari sana”
“Hatari sana kivipi?”
“Hawa ndio walikuwa walinzi wa mzee Godwin kipindi cha kampeni na waichana hawa, walikuwa magaidi wanao tafutwa, huku mwenzao mmoja akiwa ni Rahab mke wa raisi Praygod.”

Madam Mery alizungumza kwa sauti ya chinichini, huku wasiwasi mwingi ukiwa umemjaa.
“U…unataka kuniambia hawa warembo ni magaidi?”
“Ndio na kwa sasa wote wamepewa uwaziri, kwa hiyo hapo ni mawaziri”
“Mungu wangu?”
“Ndio hivyo, nchi kwa sasa inaongozwa na wendawazimu”
Gafla milio ya risasi ikaanza kusikika eneo la walilopo, katika kutazmaa tazama Eddy akawaona wanaume watatu walio jifunika nyuso zao kwa mabushori meusi, kila mmoja mkoni mwkae ameshika bunduki aina ya SMG. Wakipiga risasi hewani na kuwaamrisha watu wote kulala chini, na anaye lete ubishi anapigwa risasi.

ENDELEA
Eddy na madam Mery wakatii amri hiyo huku kila mmoja akilala chini ya sakafuni. Macho ya Eddy yakamshuhudia mmoja wasichana alio elezwa kwamba walikuwa ni magaidi na sasa ni mawaziri, akichomoa bastola yake kwenye pochi yake aliyo ishikilia. Macho ya Eddy akayaamishia kwa wavamizi hao ambao wameingia ndani ya eneo hilo. Akawaona wakianza kuwakagua mtu mmoja baada ya mwengine.

Eddy akarudisha tana macho yake kwa msichana huyo akamuona akiwa amekunja sura yake, akibabaika katika kuirekebisha risasi yake ambayo kwa haraka haraka akahisi imekwisha risasi.

“Imekata risasi”
Msichana huyo alimnong’oneza mwenzake, kwa ukimya uliopo eneo hilo Eddy aliweza kusikia sauti yake.
“Daaa na mimi sijatembea na silaha kabisa hapa”
“Oya hakuna mwenye hata magazine yenye silaha”
Sauti ya msichana huyo ambaye Eddy alitajiwa majina yao, haraka haraka ilisikika kwa mmoja wa majambazi hao, aliye geuza kichwa na kutazama watu walio lala chini ya meza.

“Oya hawa mamanzi wana wana silaha kuman**a zao”
Jambazi hayo alizungumza kwa sauti nzito huku akiikoki SMG yake tayari kwa kuwafyatulia risasi wasichana hao. Kwa haraka Eddy akaichomoa bastola yake kiunoni, kwa shambulizi la haraka ambalo hata majambazi hao hawakulitarajia, wakamshuhudia mwenzao akipigwa risasi moja ya kichwa iliyo mrudisha nyuma kiasi na kuanguka chini.

“Lu…….”
Jambazi mmoja alijikuta akikatishwa hata kutamka neno lake, alilo kusudia kumuita rafiki yake huyo, kwani risasi tatu zilitua kifuani mwake na kumuangusha chini. Jambazi aliye bakia, kwa kiwewe akajikuta akitoa magazine ya bunduki badala ya kupiga.

Akabaki akiwa ameishikilia bunduki hiyo, akampa fursa Eddy kusimama huku bastola yake ikiwa mkononi. Jambazi huyo alipo ona bunduki yake ina sua sua, akaitupa chini na kuchomoa kisu chake kirefu na kuanza kumfwata Eddy, aliye mtazama kwa umakini jinsi anavyo mfwata. Alipo karibia tu, Eddy akaruka hewani huku mguu wake wa kulia ukiachia shuti kali na zito lililo tua shingoni mwa jambazi huyo na kutupia pembeni. Jambazi huyo akanyanyuka haraka japo anayumba yumba.

Akataka kufanya shambulizi jengine, ila ngumi mfululizo zisizo na idadi, zikatua kwenye kifua chake na baadhi zikitua kwenye sura yake na kuanguka chini. Eddy akataka kumsogelea ila jambazi huyo akanyoosha mikono juu akiomba msamaha.
Mtu mmoja aliye lala pembezoni mwa jambazi huyo alipo ona jambazi huyo amesarenda, akavuta chupa yake ya bia taratibu iliyopo juu ya meza, bila ya huruma akamtandika jambazi huyo chupa ya kichwa hadi ikapasuka, kitendo kilicho mpelekea jambazi huyo kupoteza fahamu hapo hapo.

   Halima, Anna, Fetty na Agnes, wote wakatokea kumshangaa Eddy kwa ujuzi mkubwa alio kuwa nao katika kupambana. Kila mmoja moyoni mwake akajikuta akitokea kumkubali kijana huyo, ambaye hadi kwa sasa hawajamfahamu jina lake.
“Madam amka”
Eddy alimfwata madam Mery na kumpa mkono, taratibu madam Mery akanyanyuka, huku akitazama tazama kila pende, huku kila mtu aliye amrishwa kulala chini na majambazi hao, akaanza kunyanyuka kwa mtindo wa kutazama tazama kama hali imekuwa shwari.
“Umeitoa wapi bastola”

Madam Merya alizungumza kwa kumnong’oneza Eddy sikioni. Eddy hakujibu kitu cha aina gani zaidi ya kutabasamu.
“Eddy tuondoke hapa, polisi wakija wataanza kukuhoji maswali”
Wazo la madam Mery, Eddy hakutaka kulipuuzia. Wakaanza kuondoka eneo hilo kuelekea katika maeneo ya kulala, ila kabla hawajatoka eneo hilo, Eddy akastukia akiitwa na sauti ya kike nyuma yake.
“Samahani sana kaka yangu naomba kuzungumza na wewe”
Msichana huyo ni moja ya wasichana ambao Eddy alielezewa na madam Mery ambaye hakutaka kugeuka nyuma zaidi yakupiga hatua kama sita mbele na kusimama akimsubiri Eddy.

“Kwa jina ninaitwa Agnes, ni waziri wa Maliasili na utalii”
“Nashukuru kwa kukufahamu”
Eddy akajibu na kutaka kuondoka ila Agnes akamshika mkono na kumzuia.
“Samahani ninaomba kukuuliza maswali machache kama huto jail”
“Samhani dada, sipo tayari kwa kujibu maswali yako kwa sasa”
“Ok basi ninamba nikupe namba yangu ya simu”
Agnes akatoa kikadi kidogo chenye namba yake ya simu na kumkabidhi Eddy, aliye kitazama kwa sekunde kadhaa, akisoma jina la Agnes pamoja na cheo chake alicho nacho.
“Naomba unipigie simu hata kesho ninamazungumzo na wewe muhimu”

“Poa usijali”
Eddy akageuka na kuondoka na kumuacha Agnes akimtazama kwa macho ya matamanio, hadi Eddy na madam Mery wanapotea mbele ya macho yake kwa kukata kona ya kuelekea sehemu nyingine kwenye hoteli hiyo, ndipo Agnes alipo amua kurudi walipo simama wezake.
“Vipi umefanikisha”
Halima akawa wa kwanza kuuliza swali, lililo mfanya Agnes kutabasamu kidogo.
“Chezea mimi wewe”
“Ila anaonekana ana mapozi eheee?”
“Ahaaa mapozi yake yataisha mbele ya pesa, akijisumu kunipigia simu tu basi amekwisha,  nitahakikisha anakuwa wangu”
“Mmmm, ila hata mimi nimetokewa kuvutiwa naye”
Halima alizungumza huku akicheka na kumfanya Agnes kupoteza furaha na kuachia msunyo wa kukereka.
“Mmmmm mama mtu hujampata tayari umesha kuwa na wivu naye”

==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )