Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Saturday, August 19, 2017

Tundu Lissu adai kufuatwa na usalama wa Taifa kila anapokwenda

Rais wa chama cha Wanasheria Tanzania (TLS) na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu amefunguka kwa kuwataka wakuu wa vyombo vya usalama nchini wawaelekeze watumishi wao kazi za kufanya na siyo kupoteza muda na rasilimali za nchi.

Lissu amesema hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliyoitishwa na CHADEMA wenye lengo la kuzungumzia namna nchi inavyoenda kufilisika na ndipo alipomtaka Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Kamanda Modestus Francis Kipilimba na Mkuu wa Majeshi Tanzania, IGP Simon Sirro kuwapa uweledi mzuri wa kufanya kazi vijana wao.

"Mkuu wa TISS au IGP wale vijana mliowatuma wiki tatu mfululizo kunifuata kila nilipo, niliowakaba Kanisani St. Peter, muwaambie wakubwa wawaelekeze watumishi wao kutumia muda na rasilimali za nchi kupambana na wahalifu na si kuhangaika na raia wanaotimiza wajibu wao kikatiba kuwawajibisha viongozi serikalini,”  alisema Lissu.

Pamoja na hayo, Lissu ameendelea kwa kusema "Wafanye kazi ya kupambana na wahalifu na siyo kupoteza muda wao na pesa za walipa kodi kuhangaika na raia ambao wanatimiza uhuru wao wa kuiwajibisha serikali iliyoko madarakani".

Kwa upande mwingine, Lissu amemtaka Kamanda Sirro pamoja na Kamanda Kipilimba kupamba na wahalifu na wamuachie yeye kazi ya kuwajibisha waliyoko madarakani kwa mujibu wa sheria za nchi.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )