Monday, August 28, 2017

Tundu Lissu Aitisha Mgomo wa Mawikili Nchi Nzima

Baraza la Uongozi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) limewataka mawakili nchi nzima kutokwenda mahakamani Jumanne na Jumatano kama njia ya kupinga Kampuni ya Immma Advocate kuvamiwa.

Akizungumza jana Jumapili, Rais wa TLS, Tundu Lissu alisema uamuzi huo umefikiwa jana na kikao cha baraza la uongozi la chama hicho.

Alisema mawakili wote wanaotetea wananchi kwenye mahakama na kwenye mabaraza wasifanye kazi siku hiyo.

Alisema baraza hilo linafahamu kwamba wateja wao wataathirika siku hizo lakini usalama wa mawakili ni muhimu zaidi.

Lissu alisema baraza la uongozi linavitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuwahakikishia ulinzi mawakili wa Immma Advocate dhidi ya vitisho vinavyoweza kuhatarisha usalama wao.

Alisema baraza hilo linafanya jitihada za haraka za kukutana na Mkuu wa Jeshi la Polisi na Idara la usalama ili kujadiliana kuhusu shambulio hilo.

Lissu aliwataka wananchi kuhakikisha wanalinda usalama,uhuru na heshima ya wanasheria na mawakili ili waweze kutekeleza wajibu wao wa kuwatetea wananchi.

==>Lisome Tamko Zima hapo chini
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )