Monday, August 7, 2017

VIDEO: Rais wa Simba Evans Aveva na Makamu wake Geofrey Nyange Kaburu wakati wanaingia Mahakamani leo.

 Leo August 7, 2017 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kwa mara nyingine kesi ya kutakatisha fedha na kughushi inayowakabili Rais wa Simba SC, Evans Aveva na Makamu wake, Geofrey Nyange maarufu Kaburu hadi Agosti 16, 2017 baada ya upelelezi kutokamilika.
 
==>Makosa 5 yanayowakabili
1. Kughushi
Aveva alighushi nyaraka ili kujilipa deni ambalo inadaiwa aliikopesha Simba USD 300,000.

2. Nyaraka za uongo
Walitumia nyaraka za uongo ili kulipa deni kutoka benki ya CRDB.

3. Kutakatisha fedha
Tarehe tofauti Aveva na Kaburu walikula njama za kutakatisha fedha UDS 300000.

4. Kutakatisha fedha
Aveva alijipatia fedha kutoka Barclays bank tawi la Mikocheni.

5. Kutakatisha fedha Kaburu
Kaburu alimsaidia Aveva kupata pesa USD 300,000 kutoka Barclays Bank tawi la Mikocheni. 


==>Watazame hapo chini Rais wa Simba Evans Aveva na Makamu wake Geofrey Nyange Kaburu wakati wanaingia Mahakamani leo.
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )