Wednesday, August 30, 2017

Wabunge Wakerwa na Ubinafisishaji wa Kampuni ya Maendeleo ya Viwanja vya Ndege (KADCO)

Ubinafisishaji  wa Kampuni ya Maendeleo ya Viwanja vya Ndege (KADCO), umehojiwa kutokana na kile kilichoelezwa kuwa umegubikwa na utata, hali ambayo baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wametaka wapewe maelezo ya serikali, vinginevyo suala hilo litahamishiwa bungeni lijadiliwe.

Hayo yalibainika jana katika kikao kati ya wajumbe wa PAC na Mamlaka ya Usimamizi wa Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA). 

Miongoni mwa mambo ambayo wajumbe walisema yana utata, ni pamoja na CAG kubaini kuwa licha ya serikali kuwa na hisa asilimia 100 katika Kadco, kampuni hiyo imeendelea kuachiwa kuendesha Kiwanja cha ndege cha Kilimanjaro (KIA).

Utata mwingine ni hatua ya KIA kuendeshwa tofauti na viwanja vingine, kwa maana ya kuwa chini ya kampuni hiyo wakati viwanja vya ndege vingine vyote viko chini ya TAA. 

"Kwa nini hiki kiendeshwe tofauti na viwanja vingine? Na TAA wanaendesha viwanja vingine na siyo KIA... Tutamuita waziri atueleze kuna nini," alisema mwenyekiti wa kamati, Naghenjwa Kaboyoka ambaye ni Mbunge wa Same Mashariki (Chadema).

Kwa upande wake, Mbunge wa Sikonge, Joseph Kakunda (CCM) alisema: "Tuwe wazi kuwa huko serikalini kuna watu wanaendesha Kadco wanamaintain status quo kwa sababu wanapata fedha.Kama Baraza la Mawaziri halitakuwa wazi katika hili, tutawasha moto bungeni.” 

 “Kwa nini hawa TAA wawe na share(hisa) na Kadco wakati hawana mamlaka?” alisema mbunge huyo akirejea maelezo ya Mkurugenzi wa TAA katika kikao hicho aliyesema kuwa suala la Kadco haliwahusu ingawa wana hisa.

Awali, Mwenyekitiwa Bodi ya TAA, Profesa Ninatubu Lema alipoulizwa na wajumbe wa kamati kuhusu masuala kadhaa ya Kadco, alisema kampuni hiyo iko nje ya mamlaka ya TAA kwa kuwa inaripoti moja kwa moja kwa serikali.

Miongoni mwa maswali kuhusu Kadco yaliyoulizwa na Kakunda na kufanya wajumbe wengi kuchangia, ni uhusiano wa TAA na kampuni hiyo kama  wana mkataba wowote. Pia alitaka kufahamu kama kampuni hiyo, imerithiwa na serikali au imeanzishwa upya.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )