Saturday, August 19, 2017

Wanafunzi Wawili Wafariki wakichimba mchanga

Wanafunzi wawili wa Shule ya Msingi Chikomo Tarafa ya Nalasi, Wilaya ya Tunduru Mkoa wa Ruvuma wamefariki baada ya kuangukiwa na kifusi wakati wakichimba mchanga wa kujengea darasa walipokuwa kwenye mafunzo ya vitendo.

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa mkoani Rukwa SACP Gemini Mushi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kwamba  wanafunzi waliofariki ni Selina Selemani Kazembe (12) wa darasa la tatu pamoja na Sofia Sillo (9) darasa la tatu kwa kusema kuwa watoto hao waliangukiwa kwa kufunikwa na ukuta wa shimo la mchanga ambao ulikuwa ukitumika kujengea darasa.

Kamanda Mushi amefafanua kwamba "Kwa mujibu wa taarifa tulizopewa na uongozi wa shule hiyo wanafunzi hao walikuwa katika mafunzo ya vitendo yajulikanayo kama elimu ya Kujitegemea (EK).

Pamoja na hayo Kamanda huyo amesema jitihada zilizofanyika ni kuwakimbiza watoto hao katika hospitali ya Mbesa lakini kwa bahatI mbaya wakati watoto hao wanafikishwa hospitali walikuwa wameshakata roho.

Kwa mujibu wa Kamanda Mushi amesema jukumu la mazishi familia hizo zimeachiwa.
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )