Friday, September 22, 2017

JWTZ Waanza Kutekeleza Agizo la Rais Magufuli la Kujenga Ukuta Katika Madini ya Tanzanite

Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania JWTZ limeanza kutekeleza agizo la Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli la kujenga ukuta na kuweka kamera katika eneo linalopatikana madini ya Tanzanite huko Mererani.

Meja Jenerali Michael Isamuyo ametua Mererani, Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara kwa Helkopta na kukagua maeneo ambayo ukuta utaanza kujengwa mara moja. Wachimbaji na wananchi wa Manyara wamefurahia na kuahidi ushirikiano.

Rais Magufuli alitoa agizo hilo juzi alipokuwa akiwahutubiwa wananchi wa Simanjiro kabla ya kufungua barabara ya KIA – Mererani yenye kilomita 26.


Advertisement
==

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Mpekuzi Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )