Thursday, September 28, 2017

Kigwangala Aiagiza TAKUKURU Kumkamata Tabibu kwa Kutafuna Milioni 2 za CHF


Naibu Waziri wa Afya, Dk Hamisi Kigwangalla ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kumkamata tabibu, Daniel Mtatiro wa kituo cha afya Kiagata anayetuhumiwa kula Sh2 milioni za Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF).

Dk Kigwangalla aliye katika ziara mkoani Mara amekagua zahanati, vituo vya afya na hospitali ikiwa ni katika mpango wa kuboresha sekta ya afya.

Baada ya kufanya ziara katika kituo hicho cha afya, Dk Kigwangalla amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Butiama mkoani Mara, Simon Ngiliule kumsimamisha  kazi mara moja kutokana na tuhuma hizo.

Pia, ameiagiza Takukuru kumkamata tabibu huyo ili kuhojiwa na kuchukuliwa hatua. 

"Nakuagiza mkurugenzi msimamishe kazi Mtatiro na afikishwe Takukuru haraka sana. Huku ni kuhujumu mpango wa Serikali wa kuwaletea maendeleo kupitia afya matokeo yake mtu mmoja anachukua fedha za wananchi mwishowe wanakosa matibabu," alisema Dk Kigwangalla.          

Advertisement
==

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Mpekuzi Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )