Sunday, September 10, 2017

Maneno aliyosema Tundu Lissu baada ya kuzinduka

Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa (CHADEMA) Tundu Lissu ambaye anapatiwa matibabu nchini Kenya kufuatia kujeruhiwa kwa risasi na watu wasiojulikana siku Septemba 9, 2017 amezinduka na kutoa neno kwa Mwenyekiti wa CHADEMA.

Katika ujumbe amboa umewekwa na Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa unasema kuwa kiongozi huyo alipopata fahamu aliweza kutoa maneno machache akimtaka Mwenyekiti kuendeleza mapambano.

Tundu Lissu kwa sasa amelazwa nchini Kenya akipatiwa matibabu jijini Nairobi kufuatia kupigwa risasi na watu wasiojulikana akiwa Makao Makuu ya nchi mjini Dodoma siku ya Alhamis saa saba na nusu 


Advertisement
==

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Mpekuzi Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )