Friday, September 1, 2017

Mwakyembe apinga vikali uzushi juu ya ubovu wa ndege za Bombardier

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na michezo, Dk Harrison Mwakyembe ametoa agizo kwa Watanzania kupuuza maneno ya upotoshaji yanayosemwa na watu wachache hususani wanasiasa kuhusu ubovu wa ndege za Serikali aina ya Bombardier.

Amesisitiza kuupuza habari hizo kwani anaamini kuwa wazushaji hao hawana utaalamu wowote wa kutambua jambo hilo.

Mwakyembe alizungumza hayo pindi akifanya mahojiano na maalumu na waandishi wa habari akiwa katika chumba cha abiria kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Songwe akijiandaa kusafiri kwenda Dar es salaam.

Dk Mwakyembe amesema wapo watu wamekuwa wakipiga kelele za uzushi kwamba serikali imenunua ndege mbovu, jambo ambalo siyo la kweli kwani mchakato wa upatikanaji wa ndege hizo ulianza muda mrefu ukiwashirikisha wataalamu mbalimbali kwa kuzingatia mazingira ya nchi pamoja na viwanja vilivyopo.

“Kuna watu wanasema ndege hizi ni mbovu sasa watuletee za kwao ambazo siyo mbovu. Kwanza hawana hata utaalamu wa kujua ndege nzima au mbovu pia wanachoangalia ni kutumia pangaboyi tofauti na zingine lakini ubora ni uleule,”.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )