Thursday, September 7, 2017

Mwanasheria Amtaka Rais Magufuli Asaini Hukumu ya Kumnyonga Hadi Kufa Kijana Aliyeteka Watoto na Kuwaua


Mwanasheria wa kujitegemea hapa nchini Alberto Msando, amemtaka Rais Magufuli kusaini hukumu ya kunyongwa hadi kufa kwa mtuhumiwa wa mauaji ya watoto waliotekwa mkoani Arusha Bw. Samson Peter ili iwe somo kwa wengine.

Kwenye Ukurasa wake wa Instagram Alberto Msando ameandika ujumbe wa kusikitisha kuhusu vifo vya watoto hao waliotekwa na miili yao kukutwa kwenye shimo la choo mkoani Arusha, na kusema kwamba tukio alilolifanya mtuhumiwa huyo ni la ukatili wa hali ya juu, na kwamba kesi yake iendeshwe kwa haraka iwezekanavyo ili ahukumiwe na kumpa adhabu kali ikiwemo kunyongwa hadi kufa.

"Samson Peter Mungu akuadhibu, yaani huyu wala siyo wa kukaa zaidi ya miezi sita na kesi ya utekaji na mauaji!! Hii iishe hata kesho!! Na Rais asaini adhabu ya kunyongwa mpaka afe!! Naomba akihukumiwa tu Mh. Rais atengeneze historia ya kusaini kunyongwa kwake!!!", aliandika Alberto Msando.

Mwanasheria huyo machachari na maarufu Tanzania aliendelea kwa kuwataka wakazi wa Arusha kujitokeza kwa wingi katika shughuli ya mazishi ya watoto hao, ili kuwapa faraja wafiwa.

Watoto waliofariki Moureen David na Ikram Salim miili yao iliokotwa jana katika shimo la choo ambako walitelekezwa, baada ya kutekwa na mtu aliyejulikana kwa jina la Samson Peter ambaye kwa sasa anashikiliwa na polisi, kwa tamaa za fedha

Inauma sana sana kupoteza watoto hawa kwa tamaa ya fedha. Maumivu yake hayaelezeki kwa wazazi wao. Ni ukatili mkubwa sana. Jaribu kufikiria watoto hawa ndani ya shimo bila msaada wowote! Bila maji ya kunywa! Bila chakula! Baridi! Giza! Jua! Woga! Machozi! Mpaka kifo kilipowakuta!!! 😩😩😩😩! #SamsonPeter Mungu akuadhibu. Yaani huyu wala sio wa kukaa zaidi ya miezi sita na kesi ya utekaji na mauaji!! Hii iishe hata kesho!! Na Raisi asaini adhabu ya kunyongwa mpaka afe!! Naomba akihukumiwa tu Mh. Raisi atengeneze historia ya kusaini kunyongwa kwake!!! Kwa mlio Arusha atakayeweza kuhudhuria mazishi na ahudhurie!! Angalau itakuwa faraja kidogo kwa familia zao kama tutaungana kwa pamoja!! Pumzikeni kwa amani Ikram na Moureen πŸ™πŸΏπŸ™πŸΏπŸ˜”πŸ˜”πŸ˜”⚰️⚰️
A post shared by Msando Alberto (@albertomsando) on
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )