Thursday, September 7, 2017

Rais Magufuli Kupokea Ripoti ya Madini ya Almasi Leo Saa Nne Asubuhi

LEO  Tarehe 07 Septemba, 2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli atapokea taarifa ya uchunguzi wa madini ya Tanzanite na Almasi uliofanywa na kamati maalum mbili zilizoundwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai.

Taarifa hiyo itakabidhiwa kwa Rais Magufuli na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Hafla ya kukabidhiwa kwa taarifa hiyo itarushwa moja kwa moja na vituo vya redio na televisheni kuanzia saa 4:00 Asubuhi.

Wananchi wote mnaombwa kufuatilia matangazo hayo kupitia vyombo vya habari na tovuti rasmi ya Ikulu ambayo ni www.ikulu.go.tz

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )