Wednesday, September 20, 2017

Rais Magufuli ziarani Arusha Leo

Rais  John Magufuli leo Jumatano  anatarajiwa kutua Arusha kwa ziara maalumu ambapo mapema asubuhi atafungua barabara ya Kami  kutoka  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia) hadi Mererani wilayani Simanjiro.

Katika taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amesema Rais Magufuli anatarajiwa kupokewa uwanja wa ndege wa Kilimanjaro saa mbili asubuhi.

Gambo amesema  baada ya kupokelewa atakwenda Mererani Mkoa wa Manyara kuzindua barabara ya Kia-Mererani yenye urefu  wa kilomita 26.

Amesema baada ya uzinduzi huo atazungumza na wananchi na baadaye kurejea Arusha. Gambo amesema Rais Magufuli anatarajiwa kutoa kamisheni kwa maafisa waliohitimu mafunzo ya jeshi katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Jumamosi.

"Napenda kutumia fursa kuwaomba wakazi wa Arusha kujitokeza Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Septemba 23 kuanzia saa 12:30 asubuhi,"amesema.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )