Thursday, September 14, 2017

SORRY MADAM -Sehemu ya 82 & 83 (Destination of my enemies)

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA

“Jamani hii ni kama suprize kwa waziri wetu Agnes, kwa mana hakutarajia ujio kama huu wa watu katika siku kama hiiya leo”
Mshereheshaji alizungumza, akawaomba watu wote kusimama. Wakatii hadi Eddy mwenyewe. Mshereheshaji akawaalika wageni rasmi. Ambao walianza kuingia ndani ya ukumbi huo wenye mlango nyuma. Eddy na wageni wengine waalikwa wakageuka kuangalia ni wageni gani hao rasmi. Macho yakamtoka Eddy baada ya kuwaona raisi Godwin akingiia ukumbini hapo huku mbele yake akimuona John akisukumwa kwenye kiti cha matairi, na wote wakapitiliza moja kwa moja hadi kwenye meza ambayo Eddy ameketi, na taratibu raisi Godwin akampa mkono Eddy kama salam, aliye utazama pasipo kuupokea.

ENDELEA
  Taratibu Eddy akaupokea mkono wa raisi Godwin, huku akiachia tabasafu usoni mwake ambalo fika alifanani na kitu anacho kifikiria akilini kmwake. Eddy akamsalimia John kwa ishara, naye akaachia tabasamu. Msherehekaji akwaruhusu watu kuweza kukaa kwenye viti vyao na kuendelea na ratiba iliyopo mbele yao. Kwa mara kadhaa Eddy aliweza kumtazama raisi Godwin na John ambao wanaonekana hadi sasa hivi hadi sasa hawajamgundua Eddy.
“Kijana unaitwa nani?”

Raisi Praygod alizungumza huku akimtazama Eddy usoni.
“Naitwa Erickson. Erickson Forrd”
“Ahaa ninaamini unanifahamu?”
“Ndio ninakufahamu, wewe ndio raisi wetu. Mimi ni mmoja kati ya watu nilio kuwa mstari wa mbele kukupigia kampeni chuoni”
Eddya alizungumza kwa sauti ambayo sio rahisi kwa mtu kuweza kuigundua kwa haraka haraka. Uso wa raisi Praygod ukatawaliwa na tabasamu baada ya kusikia maneno ya Eddy.
“Kweli kijana?”
“Kweli muheshimiwa, nilihakikisha kwamba wanavyuo wanakuchagua na kuhitaji mabadiliko ya kisiasa. Hatuwezi vijana tangu tunazaliwa tuwe tunatawaliwa na chama kimoja”
“Unachukua fakati gani?”

“Nachukua utawala bora”
“Ahaaa, sawa sawa. Hivi unauonaje uongozi wangu?”
“Kusema kweli machoni mwa watu wengi wanaweza kusema uongozi wako unamapungufu. Ila kwa sisi waelewa tunaelewa uongozi wako ni mzuri kwa maana serikali yetu inapunguza matumizi ambayo si ya msingi. Kwa mfano hili swala la kutaka kuibadili nchi na kuwa nchi ya kifalme, ninakuunga mkono wa asilimia mia”

Eddy alizungumza kwa kuajiamini na kumfanya raisi Godwin kuzidi kufurahi pasipo kugundua kwamba Erickson Forrd ndio Eddy Godwin mwanaye wa pekee wa kiume ambaye ni adui yake namba moja.
“Unajua muheshimiwa, ukiweka nchi kuwa na uongozi wa kifalme, tutapiga hatua kubwa ya kiuchumi. Tazama Uingereza hadi leo wanamilikiwa na Malikia. Tazama uchumi wao ulipo kwa sasa. Wapo mbali sana muheshimiwa, na mimi ninazidi kukuunga mkono hata chuoni nitahakikisha kwamba uongozi unabadilika”
Muda wote Eddy akizungumza John alimtazama kwa umakini mdomoni mwake, akataka kuzungumza kitu ila akanyamaza.

“Unaonekana upo vizuri kijana”
“Kidogo tu muheshimiwa”
“Na unasoma chuo gani?”
“Ninasoma Mlimani”
“Ahaaa kumbe ni hapa hapa Dar es Salaam”
“Ndio muheshimiwa”
“Basi nitafanya mawasiliano na wewe ili tuyazungumze mengi”
Raisi Godwin kwa ishara akamuita mlinzi wake na kumnong’oneza kitu. Mlinzi wake akatoa kadi ya mawasiliano na kumkabidhi raisi kisha raisi Godwin akampatia Eddy.
“Tutawasiliana kijana hii ni namba ya simu yangu ya mkononi”
“Asante sana muheshimiwa”
“Hivi umesema unaitwa nani?”
“Erickson Forrd muheshimiwa”
“Jamani naona mtoto wetu leo anahitaji kuzungumza kitu, ngoja nimpatie maiki”

Mshereheshaji alizungumza na kuwafanya Eddy na raisi Godwin kuangalia alipo Agnes, aliye kabidhiwa maiki namshereshaji. Agnes akasimama kwenye kiti huku macho yake akimtazama Eddy aliye kaa meza moja na raisi Godwin.
“Napenda kuwashukuru jamani kwa kuweza kunifanyia sherehe hii, ambayo siku ya leo kwangu ni muhimu sana kwangu. Nikisema niwataje mmoja mmoja basi nahisi nitataja ukumbi mzima. Ila kusema kweli shukrani yangu inatoka ndani ya moyo wangu.”

Agnes alizungumza na kuwafanya watu wote ndani ya ukumbi kuwa kimya na kuendelea kumsikiliza kwa kile ambacho anakizungumza.
“Katika maisha yangu, naamini rafiki zangu wa karibu hawajawahi kusikia wala kuniona nikiwa nina mchumba. Ila leo ninahitaji kuwaeleza hili. Nina mchumba  wangu na yupo hapa, nitakapo mtaja basi nitaomba aje hapa mbele watu wote mumuone”
Eddy kidogo mapigo ya moyo yakamuenda kasi kidogo ila akajikaza na kujidai kama sio yeye ambaye atakwenda kutajwa.
“Laazizi wangu, Asali wangu, mume wangu mtarajiwa Erickson Ford popote ulipo ninakUomba unyanyuke”
Watu wote wakaanza kutazama tazama, raisi Godwin na John wakabaki wakimkodolea macho Eddy waliye kaa naye kwenye meza moja.

“Kumbe ni wewe bwana mdogo?”
Raisi Praygod alizungumza huku akitabasamu na kumtazama Eddy aliye achia tabasamu pana. Eddy akatingisha kichwa na kusimama taratibu, akaanza kupiga hatua za taratibu hadi alipo kaa Agnes, aliye mkumbatia kwa muda kisha akamuachia. John sura yake dhairi ikaonyesha kujawa na hasira kwa kitendo hicho hadi raisi Godwin akakigundua.
“Vipi mbona umekasirika ?”
“Ahahaa hapana muheshimiwa”
John alizungumza kwa kuzuga, ila kusema kweli moyoni mwake kwa haraka ametokea kumchukia Erickson Forrd, hii yote ni kutokana na hisia za mapenzi alizo kuwa nazo juu ya Agnes, ila ukaaji kimya wake ndio ulio mponza.
‘Erickson Forrd lazima nikuue’

John aliwaza huku akimtazama Eddy jinsi anavyo lishwa kipande cha kike na Agnes. Si John peke yake bali hata Manka aliyte kaa viti vya nyuma kidogo hasira kali, ikazidi kuutesa moyo wake, kwa mara kadhaa akawa anafikiria ni jinsi gani anavyo weza kumuangamiza Agnes ili kubaki na Erickson Forrd peke yake.
‘Lazima nimuue, Erickson ni wangu. TENA WANGU PEKA YANGU’
Manka alizungumza huku machozi yakimlenga lenga, kiasi kwamba akatamani anyanyuke na kwenda kuwatengenisha Erickson na Agnes wanao pigana mabusu kiholela holea. Sherehe ikazidi kuendelea hadi ikafikia tamati. Raisi Godwin akawafwata Eddy na Agnes walipo simama kwa ajili ya kuwaaga.

“Agnes hongera, umechagua kijana mzuri sana”
“Asante sana muheshimiwa nakushuru sana kwa kuweza kuhudhuria”
“Usijali, unajua nilikwenda Marekani kwa ajili ya mapumziko, ila Manka alipo nieleza juu ya sherehe yako ikanilazimu jana turudi”
“Asante sana muheshimiwa, umenipa nafasi ambayo ni ya pekee sana”
“Usijali wewe ni kati ya watu ninao waheshimu na kuwajali sana, ingeuwa si vyema kama leo nisinge weza kuhusika katika hafla hii, naamini usinge jisikia vizuri”
“Hapana muheshimiwa, mimi ni muelewa kwa maana sikutegemea kabisa ujio wako”

“Usijali, Erickson Forrd ngoja mimi niwaache mukapumzike. Ila kesho wasiliana na mimi na kama ikiwezekana njooni  wote ikulu tuzidi kuyajenga”
Raisi Praygod alizungumza huku akimpa mkono Eddy, ambaye kwa haraka akaupokea huku akiwa na furaha kubwa ambayo furaha yote ni feki, kwani kisasi na chuki dhidi ya mzee Godwin imejaa moyoni mwake.
“Asante sana muheshimiwa nina amini bibie atanileta”
“Haya ngoja tuondoke nawatakia usiku mwena”
“Nawe pia muheshimiwa raisi”

Eddy akamtazama kwa macho makali jinsi raisi Praygod wanavyo ongozana na John anaye sukumwa kwenye kiti cha matairi na mlinzi wake.
“Honey mbona umewakazia macho”
“Ahaa hapana honey katika maisha yangu sijawahi kuonana na raisi uso kwa uso”
“Kweli mpenzi wangu”
“Kweli siwezi kukutani, leo ndio mara yangu ya kwanza”
Eddy aliongopea ila anacho kijua moyoni mwake ni kulipiza kisasi dhidi ya Mzee Godwin pamoja na John ambaye amepunyuka punyuka katika kisasi cha kwanza alicho kuwa anahitaji kuweza kumfanyia.  Agnes na Eddy wakaondoka na kuelekea katika hoteli walio lipiwa kama zawadi ya kwenda kustarehe kwa siku mbili mfululizo.
                                                                                                                   ***
   John njia nzima akiwa kwenye gari pamoja na mlinzi wake aliwaza ni jinsi gani ya kumuuErickson Forrd, kwa maama ameingia katika kumi na nane zake.

“Ninakazi ambayo ninahitaji kukupatia”
John alimuambia mlinzi wake, kwa sauti iliyo jaa mikwaruzo mingi dhairi akionekana kusumbukiwa na jambo fulani moyoni mwake ambalo hakulihitaji kuliweka wazi kwa mtu yoyote kwani, katika maisha yake hakuwahi kujikuta akiingia kwenye hisia hali za mapenzi kama alizo hizo.
“Kazi gani bosi?”
“Ulimuona yule kijana anaye itwa Erickson Forrd?”
“Ndio bosi nilimuona”
“Nahitaji umfwatile hatua kwa hatua, kila detail zake ninaomba uniletee”
“Sawa muheshimiwa”
“Na akionekana humuelewi, hakikisha unampoteza”
“Sawa mkuu”
                                                                                                                    ***
   Si Phidaya wala Shamsa aliye weza kupata lepe la usingizi, kila mmoja akili yake ameielekezea kwa Eddy. Kila mmoja aliamuwazia jinsi Eddy anavyo banjuka na mwanamke ambaye anaye kwa usiku huo. Shamsa maumivu aliyo yapata yaliweza kujidhihirisaha hadi usoni mwake na kumfanya Sa Yoo kuweza kumuuliza ni kitu gani kinacho endelea.
“Ahaaa wee acha tu”
“Si wezi kuacha tu, ikiwa ninakuona unajambo ambalo linakusumbua. Ni vyema tuzungumze kwa pamoja kama ni mawazo niweze kukusaidia”
“Sa Yoo si kila jambo ni la kukushirikisha wewe, mengine ni mambo binafsi”

Shamsa alizungumza huku kwa mbali machozi yakimlenga lenga. Sa Yoo akaka kitako kitandani, akamuangalia vizuri, taratibu Sa Yoo akashuka kitandani na kwenda hadi sehemu ilipo swichi, akawasha taa na kurudi kurudi kitandani.
“Shamsa nakuomba uzungumze, ni nini kinacho kusumbua eeheee”
Sa Yoo alizungumza huku taratibu akimnyanyua Shamsa kutoka kitandani. Kichwa cha Shamsa akakiweka kwenye bega lake..
“Niambie sasa, ni nini kinacho kusumbua rafiki yangu?”
“Ni Eddy”
“Eddy kafanya nini?”
Shamsa akashusha pumzi kidogo huku akijifuta machozi usoni mwake.

“Eddy ana mwanamke mwengine”
“Sasa Shamsa huyo mwanamke ambaye anaye si anatusaidia katika kuikamilisha kazi yetu”
“Ndio Sa Yoo, ila roho yangu inaniuma”
“Inakuuma kwa nini sasa?”
“Bado ninampenda Eddy, huyu ndio Black Shadow wangu. Upendo wangu kuondoka kwake ni ngumu kama unavyo fikiria”
Sa Yoo akajikuta akishusha pumzi kidogo huku akimtazama Shamsa anaye endelea kutiririkwa na machozi.
“Lakini Shamsa, si umesha ufahamu ukweli kwamba Eddy ni baba yako, inakuwaje sasa bado una hisia za mapenzi juu yake?”
“Hata kama ukweli ni kwamba tayari amesha nivunja bikra yangu?”
“NI NANI AMEKUVUNJA BIKRA YAKO?”
Sauti ya Phidaya ikawastua wote na kujikuta macho yao wakiyaekekezea mlangoni, na kumuona Phidaya akiwa amesimama huku akiwa amevalia nguo zake za kulalia.
                                                                                                                 ***
    Asubuhi na mapema Eddy akawa wa kwanza kuamka kitandani, moja kwa moja akaelekea bafuni, akaoga kisha akarudi chumbani akavaa nguo zake alipo hakikisha amemaliza, akamtazama Agnes kwa muda akamtingisha huku anamuita.
“Honey honey”
“Mmmmmmm”
Agnes aliitika kivivu huku akijigeuza kitandani na kumtazama Eddy usoni.

“Nahitaji kwenda nyumbani kwangu mara moja”
“Kwa nini jamani, wakati tunakaa hapa siku mbili”
“Nalitambua hilo mpenzi, nakwenda kuchukua nguo. Unahisi ikulu tutakwendaje”
“Mmmm kama ni hivyo tutakwenda kununua madukani”
“Mmmm honey kuna vitu nahitaji kuvikamilisha asubihi ya leo kisha nitatarudi kabla ya saa nne asubuhi”
“Sawa naomba unibusu”
Eddy taratibu akamuinamia Agnes na kumbusu mdomoni.
“Usichelewe mume wangu”

“Sawa”
Eddy akatoka chumbani, akaingia kwenye moja ya lifti iliyopo hapo gorofani. Akashuka hadi chini moja kwa moja akaelekea kwenye gari lake.  Kitu cha kwanza kukifanya akaiwasha simu yake, kwa haraka akaitafuta ni sehemu gani ilipo namba ya raisi Praygod, akampigia.
“Habari za asubihi muheshimiwa?”
“Salama, vipi mpango waku upo vipi?”
“Nimefanikiwa kuonana na raisi Godwin, cha kumshukuru Mungu hajanistukia. Na kikibwa zaidi amenipatia namba yake ya simu”

“Kweli?”
“Ndio muheshimiwa na hapa amehitaji leo niweze kwenda ikulu kuonana naye”
“Safi sana ni mwanzo mzuri ninaimani kazi inakwenda kuwa rahisi kwa upande wetu”
“Ni kweli hapa nahitaji kurudi huko nibadilishe nguo, kisha nionana na huyu mwanamke, ila mke wangu nikionana naye nahisi uchungu mwingi moyoni mwangu”
“Basi usirudi nyumbani cha kufanya tuonane Mlimani City tuzungumze”
“Kwa nini nisirudi?”
“Kwa maana ukimuona Phidaya unaweza kushindwa kuifanya kazi yako, na kumbuka kuna shambulizi leo limepangwa kufanywa kwenye onyesho la huyo msanii”
“Kweli muheshimiwa nitajitahidi kuhakikisha halifanikiwi”
“Sawa tuonane Mlimani City”

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )